RC Chalamila awataka wakazi wa Mwanza kunywa pombe ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, asema baadhi ya baa kuwa na kelele za muziki ni sawa

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535


MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi za serikali.

Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodiza serikali.

Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.

Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.

Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.

Mkuu wa huyo wa mkoa baada ya kukabidhiwa ofisi, alianza ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.
 
Point wacha tu tunywe maisha yenyewe mafupi hivi jiwe tumemzika hata urais ajaufaidi vizuri.

Wacha tulewe tu maisha ni mafupi sana pesa tumeshatafuta na tunaendelea kutafuta halafu tufe tuziache ..

Kelele maana yake ulichagua mwanza kuna maeneo mengi sana yasiyo na usumbufu wa kelele

Kama Kiseke, Buswelu usagala, Nyasaka,Kiloleli, Nyamongoro na maendeo mengine mengi

Uza kwenye kelele kajenge kwenye utulivu.

Yupo sahihi 100%.
View attachment 1800253
 
Naunga mkono hoja baa Zingine wauze 24 hours serikali ikusanye kodi ya kutosha

Yupo sahihi 100% kwa mtazamo wangu
Ndo maana watu wanamuona kama tahira fulani. Masuala ya kelele na kero zake bado anasema ni sawa. Kwa nini hizo kelele zisumbue wasiokunywa pombe. Chalamila kumbe kweli kubwa jinga ili jamaa
 
Atleast leo kaongea kitu..ila swala la kelele kwa bar zilizokaribu na makazi ya watu ni za kuangaliwa.

Watu wanywe BEER..
Swala la kelele wakiliingiza tutaingia hadi haya makanisa ya uswahili yanayokesha.
 
Kunywa safari lager,huku ukifurahia jagwa,bila kusahau chimbwanga na ule mjani lager pembeni
Nalog off
 
Kama kanyongeza ka mshahara na posho ni hadi kukunjana mashati, nani atakuwa na jeuri ya kuweka kikao hata cha nusu saa bar......ndo maana tunashuhudia bar zimebaki viti vitupu na hii imeenda kuua ajira za wahudumu wa bar na wajasiriamali wengine kama supu na nyama choma.
 
Huyu anafaa sana kuwa RC wa Kilimanjaro
 
Wewe na chalamila akili zenu zinafana!! ona hata ulivyoandika!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…