RC Chalamila awataka wakazi wa Mwanza kunywa pombe ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, asema baadhi ya baa kuwa na kelele za muziki ni sawa

View attachment 1800234

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi za serikali.

Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodiza serikali.

Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.

Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.

Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.

Mkuu wa huyo wa mkoa baada ya kukabidhiwa ofisi, alianza ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.
Yupo kwa meko.bado
 
Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.
Stupid!!!

Haangalii madhara kwa watu wengine yeye anaangalia mapato na siyo ustawi wa familia za watu
 
Huyu alipanga kumchonganisha mama na mola wake. Mama haombi kuombewa. Anaomba mwenyewe.
 
Back
Top Bottom