Serikali ya mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na kampuni ya Heineken Beverages International imetangaza kuandaa Carnival ya bia ya mwisho wa mwaka iliyopewa jina la 'Bata la Disemba' ambapo wananchi na wadau mbalimbali watakutana kwa pamoja kufurahia bata hilo linalotarajiwa kufanyika kuanzia Disemba 6 hadi 8.2024 katika viwanja vya Leaders club
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametangaza hilo hapo jana, Jumatatu Novemba 25.2024 alipokutana na wanahabari Serena Hotel, Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo mengine amesema Carnival hiyo ni sehemu ya maadhimisho ya kuimarika kwa uhai wa kiuchumi wa jiji la Dar es Salaam