Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Akizungumza na viongozi mbalimbali wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa huo, Albert Chalamila amesema ucheleshwaji wa maboresho ya Barabara unaoendelea hauna taswira nzuri kwa kuwa mikataba ilisainiwa na sherehe ikafanyika.
Anasema “Tulisaini mkataba na tukafanya sherehe ya ujenzi wa Barabara ya Kimara – Bonyokwa kule Segerea, kama tulijua tunaweza kuchelewa kidogo tungeishia kusaini mkataba na ile sherehe ingesubiri kidogo ambayo tuliifanya mbele za watu.
“Barabara nyingine ambayo ina umuhimu mkubwa sana na tumeishaisema sana ni ya Kibada – Mwasonga (Kimbiji), nitafanya maombi kwa Waziri (wa Ujenzi) ili wajumbe wafuatao waende katika kikao cha haraka, mwakilishi wa Wabunge, Mwakilishi wa Madiwani, Wataalam wakiwemo Meneja wa TANROADS.
“Nitazungumza naye kuhusu ucheleweshwaji wa Miradi ya DMDP ambayo Rais alishatoa maelekezo namna inavyotakiwa kufanyika pamoja na Barabara zilizo chini ya TARURA na TANROADS.”
Ikumbukwe Aprili 29, 2024, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa aliwahakikishia Wananchi kuwa Serikali iko kazini na imejipanga kikamilifu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, TANROADS na TARURA kurekebisha maeneo yote yaliyopata athari ili ziendelee kupitika na kutokwamisha shughuli za wananchi na viwanda katika uzalishaji.
Bashungwa alimuelekeza Mkandarasi Estim kuendelea kuleta vifaa na mitambo yote katika eneo la mradi wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji wakati akisubiria malipo ya awali na kiangazi kianze ili ujenzi uweze kuanza mara moja.
Siku hiyo pia, Mbunge wa Kigamboni, Dkt. Faustine Ndugulile alisema Barabara ya Kibada - Mwasonga hadi Cheka inapitisha magari zaidi ya 1,000 ya ujazo mbalimbali makubwa na madogo na pia inaelekea kwenye viwanda vikubwa zaidi ya 10 na kuna eneo kubwa la uwekezaji hivyo ujenzi wa barabara hiyo utaleta tija na chachu ya kimaendeleo kwa wanakigamboni.
Aidha, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. John Mkumbo ameeleza kuwa ujenzi wa barabara ya Kibada - Mwasonga - Kimbiji (km 41) utatekelezwa na Mkandarasi wa Kampuni ya Estim na tayari ameshakabidhiwa eneo la ujenzi tangu Aprili 10, 2024.