RC Chalamila: Haiwezekani Watu wakakesha kwenye Ibada au Baa kila siku, uzalishaji utafanyika Saa ngapi?

RC Chalamila: Haiwezekani Watu wakakesha kwenye Ibada au Baa kila siku, uzalishaji utafanyika Saa ngapi?

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, amewakata wamiliki na wafanyabiashara wa Baa kufanyabiashara zao kwa mujibu wa sheria na taratibu za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC)

Akizungumza kwenye kikao na baadhi ya wamiliki na wafanyabiashara wakubwa wa Baa katika Wilaya ya kinondoni Julai 14, 2026 amesema miongoni wa taratibu hizo ni pamoja na kuhakikisha maeneo ya biashara zao hayana makelele yanayovuka nje ya maeneo yao ya kibiashara.

"Leo tumeitana kama sehemu ya awali ya maonyo niwape wiki moja ya kuhakikisha mabadiliko yanafanyika haiwezekani watu wako wanakuwa kwenye ibada kutoka saa 12 asubuhi mpka kesho asubuhi watazalisha saa ngapi na haiwezekani mtu anakaa anakunywa Bia kutoka saa 12 asubuhi hadi 12 asubuhi lazima achukuliwe apelekwe Muhimbili,"- RC Chalamila

Mambo ya kipuuzi sana, nchi inarudishwa miaka ya 70!
Kwani niclazima kila mtu arudi nyumba ni kulala!?
 
Hiwezekani mtu akae guest house na mwanamke kuanzia saa 12 asubuhi mpaka saa 12 jioni, hili amelisahau Muheshimiwa
 
Watu wanapotumia vipato vyao kupombeka wasipangiwe masaa, kwa vile fedha ni zao na wananoa akili za kutafuta fedha zaidi. Ilimradi mtu hadhuru watu wengine.

Na pia kadiri wanavyopombeka zaidi, TRA hupata zaidi. Wanastahili kupongezwa. badala ya kubugudhiwa.
 
Gentleman walizidi nikiwa KABAGHO mziki wao ni maradufu Juzi naona wamepunguza sauti,

Tufungulie hizo baa tushakosa kazi muheshimiwa wengine tunachoma nyama loose Nut umemuona kant ombe akitafuta mabwana
 
Huyu pimbi hajui bar ndio inakesha sio walevi/wanywaji

cha muhimu hapo ni kupunguza makelele hasa wanaokesha makasani!
 
Kiwango cha wastani wa pato (mapato) yatokanayo na unywaji na mauzo ya bia hapa nchini hufikia takriban Dola za Marekani bilioni $1.15 hadi $1.4 bilioni (sawa na zaidi ya Tsh Trilioni 3) kwa mwaka. Pato hili huchangiwa kwa kiasi kikubwa na kampuni kama Tanzania Breweries Limited (TBL) na Serengeti Breweries Limited.

anataka kuwahujumu TRA
 
Ameshakosa kazi za kufanya huyu msomi mjinga.
Ni lini yeye na ulevi wake alikuta bar wanagawa bia bure!!?
 
Back
Top Bottom