Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila akizungumza kwenye sherehe za kuweka Wakfu jengo la Ibada la Kanisa la Waadventista wa Sabato Magomeni, leo Disemba 15, 2024.
"Mkoa wa Dar es Salaam uko salama, hizo habari zinazosambaa za mtu kutekwa sio za kweli na hivi karibuni mtasikia wenyewe nini kilisababisha apotee"
Pia, Soma: Mke wa Ulomi asimulia sakata la kupotea kwa mumewe
Kufuatia taarifa zinazozagaa mitandaoni, Jeshi la Polisi limetoa ufafanuzi kwa mujibu wa ushahidi uliokusanywa.
Vincent Peter Massawe, ambaye taarifa za kupotea kwake ziliripotiwa tarehe 19.11.2024, alithibitishwa kuwa na harusi tarehe 16.11.2024. Baada ya harusi, aliazima gari aina ya Toyota Ractis (T.642 EGU) kwa shughuli hizo lakini hakulirejesha. Badala yake, tarehe 18.11.2024, aliuza gari hilo kwa shilingi milioni tisa, akalipwa milioni nane, na kiasi kingine alituma kwa mke wake kulipia madeni ya harusi.
Gari hilo limekamatwa, na ushahidi unaonyesha Massawe pia anadaiwa na watu wengine jumla ya shilingi milioni 69. Uchunguzi unaendelea kubaini ukweli wa tukio hili, na taarifa rasmi zitatolewa baada ya mahojiano zaidi, hasa na mke wake, ambaye inaaminika ana taarifa muhimu.