RC Chalamila kaonewa bure ruhusa ya magari binafsi kutumia barabara ya mwendokasi, Mchengerwa angepambana na Bashungwa

RC Chalamila kaonewa bure ruhusa ya magari binafsi kutumia barabara ya mwendokasi, Mchengerwa angepambana na Bashungwa

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Wakuu, siku ya jana Waziri wa TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa alimtolea povu Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam kuwa hana mamlaka ya kutoa ruhusa ya magari kutumia njia ya mwendokasi. Ilikuwa kama udhalilishaji fulani njia aliyotumia waziri huyo kufikisha ujumbe. Soma karipio la Mchegerwa Mchengerwa achukizwa na maamuzi ya RC Chalamila, ahoji ametoa wapi mamlaka?

Ikumbukwe kuwa RC Chalamila alifanya vile baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi wa wakati ule, Innocent Bashungwa, hivyo Mchengerwa alichofanya haikuwa sawa kimaadili na kiuongozi. Soma Bashungwa aruhusu magari binafsi kutumia barabara za mwendokasi ambazo hazijaanza kutumika

 
Kweli ww chawa mbona uyo Boss wako RC wakati anamjibu yule mjamzito ukotoa bandiko hapa.? Takataka kabisaa.
Fisiem ni fisiem TU
KAZI ni kipimo cha utu
 
Tz hatuna mpangilio mzuri wa uongozi kila mtu anafanya anavyoona vema machoni pake hasa awamu hii inayomalizia miaka ya magufuli
 
Wadhibiti kwanza hawa wenye magari ya vingora wamekuwa kero kubwa. Kila STK. Dfp na hizi namba za singapore wanajifanya wana haraka kuliko watu wote.

Nashauri majaji wapewe nyumba masaki ili wawahi ofisini
 
Back
Top Bottom