informer 06
Senior Member
- May 11, 2024
- 184
- 170
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ameagiza maeneo yote ya wazi (Open Spaces) yaliyopo katika Wilaya ya Kinondoni kupatiwa Hati za Umiliki ili kuweka utaratibu wa kisheria wa umiliki na matumizi yake.
Chalamila ametoa agizo hilo Septemba 23, 2026 alipofanya ziara katika eneo la wazi la Uwanja wa Josho la Mbwa, Oysterbay Wilayani Kinondoni alipokwenda kufuatilia hali ya matumizi ya eneo hilo.
Amesema mazoea ya kumiliki na kutumia maeneo ya wazi bila ya kuwa na hati halali yanapaswa kuachwa mara moja, amesisitiza kuwa hati zitasaidia kuthibitisha uhalali wa maeneo hayo na kuhakikisha yanatumika kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na Serikali.
"Hatutakubali kuona maeneo ya wazi yakimilikiwa kiholela, kila eneo lazima liwe na hati. Hii itaondoa migogoro na kulinda maeneo haya kwa manufaa ya wananchi wote," amesema Chalamila.
Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo Saad Mtambule, alipokea agizo hilo kwa niaba ya Viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni na kuahidi kulitekeleza ipasavyo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Halmshauri ya Manspaa ya Kinondoni ni kwamba ziara hiyo ni sehemu ya jitihada za Mkoa kuhakikisha maeneo ya wazi yanatunzwa, yanalindwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.