RC Chalamila: Mnyonge anafurahia vitu vya ovyo ovyo

RC Chalamila: Mnyonge anafurahia vitu vya ovyo ovyo

Kama unaona dar kuna kufoleni hamia kijijini....dr.chalamila
 
Huyu mjomba wangu huwa simuelewi....kabisaa......sijui ana shida gani ? Nadhani huyu aende Lindi au Singida huko Dar sidhani kama ana ubunifu kwa jiji hili......hapanaa
Halafu mara nyingi wanatumia lugha za kitoto sana, ni kama vile haushirikishi vyema ubongo wake
 
Lusungo Lakini wenzake huwa Wanasema CCM ni chama cha wanyonge. Sasa itakuwaje???
Nadhani wanyonge wanao zungumziwa hapo ni wanyonge wanao kipigia kura ...maana ni kweli wanyonge ndiyo wanao kipigia kura ...kwa maana kuna (wapiga kura wa ccm) na (wamiliki wa ccm).....wamiliki wa ccm siyo wanyonge
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, amesema kuwa mtu mnyonge hawezi kufurahia kitu kizuri, mnyonge anafurahia vitu vya hovyo hovyo.

Chalamila amesema maneno hayo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi, wafanyabiashara, na viongozi mbali mbali kwenye Machinjio ya Vingunguti siku kadhaa zilizopita.

"Ukiona Mheshimiwa Rais anajenga soko zuri, hajengi Kwa sababu kuna mnyonge..." Alisema Chalamila.

Wanyonge mjipange kivingine ukweli ndiyo mshaambiwa hivyo.

Chanzo: Global Tv.
Mwenda zake alitugeuza na kutujaza ujinga wa "UNYONGE" na kijinga kabisa tukaupokea unyonge wa kuvishwa kipumbavu kabisa.
Baadhi ya vitu vya ovyo ovyo ambavyo mnyonge anaweza kufurahia ni tajiri au boss wake kufilisiwa alhali yeye mwenyewe anafanya kazi ktk ofisi ya boss huyo huyo anayefilisiwa, kwa Upumbavu wa mnyonge hatambui kwamba ajira yake ITASIMAMA.
 
Mkuu tupe tafsiri halisi ya neno 'mnyonge' ili tuwe na uelewa wa pamoja wakati tukijadili hoja hii!
Twaweza pata tafasil halisi ya neno mnyonge chato pekee ambako neno hili liliasisiwa. RAIS WA wanyonge
 
Au alitaka kumaanisha kuwa wanyonge hawana faida kwa Taifa linapokuja suala la uwekezaji kiuchumi???
 
Back
Top Bottom