RC Chalamila: Nikikuta uchafu mbele ya duka lako utalala selo kwa saa 48

Mpaka Rais aseme Dar es Salaam ni chafu na yeye ndio ajitokeze na vitisho?
Ukiacha hilo la Chalamila kutenda baada ya rais kusema....
Yeye RC alitaka uchafu unaokusanywa na maduka uwekwe wapi kama siyo nje ya duka husika?
Alitaka wenye maduka wahifadhi ndani uchafu wanaozalisha badala ya kuweka nje ?
Kama uchafu uliowekwa nje hauzolewi na gari za taka,hilo siyo tatizo la wenye maduka,ni tatizo la waliopewa tenda kukusanya taka jijini.
Isitoshe,RC hana mamlaka ya kumuweka ndani mtu yeyote kisheria. Kisheria ni polisi ndiyo huomba kumuweka mtu mahabusu kwa muda huo endapo wanataka kuendelea kufanya naye mahojiano au kw masuala ya kiusalama.
Inakuwa hivi....,polisi wanapeleka ombi lao kwa hakimu ambaye husikiliza nakuamua kama sababu za polisi za kumuweka mtu husika selo kwa muda uliotajwa. Endapo sababu za polisi zina mashiko,ndipo hakimu hutoa udhuru kwa kutoa kwanza taarifa kwa RC au DC ambao kazi yao ni kupitisha tu,lakini kiufundi wakuu wa mikoa hawatoi amri hiyo wao. RC na FC ni wanasiasa, na suala la ukamataji wa watu ni suala la kisheria.
 
Huyo ndiyo RC anayetakiwa, huwezi kumbembeleza mtu mwenye akili zake na akitoka hapo ataanza kuitukana Dsm kwamba inanuka. Napenda viongozi km Chalamila na Mnyeti
 
Kwani uchafu unahusianaje na mvua za El-nino?
 
Huyo ndiyo RC anayetakiwa, huwezi kumbembeleza mtu mwenye akili zake na akitoka hapo ataanza kuitukana Dsm kwamba inanuka. Napenda viongozi km Chalamila na Mnyeti
Watu wanakaa na uchafu wiki 2 hadi 3 mpaka gari la taka lipite,wakati kawaida huko ilikuwa kila jumamosi gari la taka ilitakiwa kupita
Huku watu kila mwezi wanalipa kodi ya taka
Angalie na hilo na huko kwenye dampo watatue changamoto

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…