RC Chalamila: Nimemwandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda aitishe kikao cha wadau kujadili bei ya Saruji!

RC Chalamila: Nimemwandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda aitishe kikao cha wadau kujadili bei ya Saruji!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amemtaka Katibu mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara kuandaa kikao cha wadau wa Cement kujadili bei ya bidhaa hiyo.

Chalamila amesema Mbeya wamefanikiwa na bei ya Cement haijapanda hivyo anataka ubunifu wake utumike katika level ya taifa ambapo wasafirishaji Cement ni sekta muhimu ya kujadiliana nao kumaliza kadhia hii.

Chanzo: ITV habari!
 
Bad kama hivyo atakuwa ni mchumi mzuri,natoa wazo tumwombee apate teuzi husika aweze kutuliza hali ya soko kupitia matamko,ubunifu na mbinu nyinginezo.
Hahahaha na BA. Kiswahili
 
Huyu bwana mdogo ni half cooked.
Hajui wala haelewi dynamics za production, Cement supply, na demand.
Haelewi kuwa supply lines za mikoa mingine zimekuwa ngumu kutokana na matatizo ya kiwanda cha Dangote.

Kiwanda cha Saruji Mbeya kiko hapo hapo Mbeya naye anaona ni muujiza wa kijanja bei haijapanda!

Pengine vile vile atabaki kushangaa kwa nini ma Chef(wapishi) wengi wana vitambi!
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amemtaka Katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara kuandaa kikao cha wadau wa cement kujadili bei ya bidhaa hiyo.

Chalamila amesema Mbeya wamefanikiwa na bei ya cement haijapanda hivyo anataka ubunifu wake utumike katika level ya taifa ambapo wasafirishaji cement ni sekta muhimu ya kujadiliana nao kumaliza kadhia hii.

Source ITV habari!
Bei ya vitu haiamliwi kwa vikao na wadau sijui watu gani,haihitaji maguvu ya serikali,fanyeni mazingira ya uwekezaji na ufanyajinkazi yawe rafiki,tofauti na hapo mtakuwa mnaonea watu tu.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amemtaka Katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara kuandaa kikao cha wadau wa cement kujadili bei ya bidhaa hiyo.

Chalamila amesema Mbeya wamefanikiwa na bei ya cement haijapanda hivyo anataka ubunifu wake utumike katika level ya taifa ambapo wasafirishaji cement ni sekta muhimu ya kujadiliana nao kumaliza kadhia hii.

Source ITV habari!
Huyo akapimwe kwanza akili ndiyo aendelee kurohoja,au analazimisha uwaziri?
 
Bad kama hivyo atakuwa ni mchumi mzuri,natoa wazo tumwombee apate teuzi husika aweze kutuliza hali ya soko kupitia matamko,ubunifu na mbinu nyinginezo.
Akili zake ndiyo zinavyo mtuma
 
Back
Top Bottom