RC Chalamila: Ukiona una miaka 40 na huna hela, usimlaumu Rais wa Jamhuri

Replica

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Posts
1,681
Reaction score
8,887
Mkuu wa Mkoa wa Dar, bwana Chalamila akiwa Ikulu leo amesema ukijiona una miaka 40 au zaidi na huna hela usimlaumu Rais kwani unakuwa umezaliwa wakati wa Mwalimu na katikati vimepita vipindi vingi vya uongozi, akidai kwanini alaumiwe mtu mwenye miaka mitatu kwenye uongozi.

Chalamila amesema wajibu wa Serikali ni kuandaa mazingira yatayokuwa rafiki ili kumsaidia mtu kuchemka na fursa ambazo zimeshaletwa na Serikali.

Chalamila amemaliza kwa kusema lawama ni tamko la laana linalofanya mtu ajisahau pale alipokosea na kutojisahihisha akidhani yupo alivyo kasababu ya sababu ambazo sio kweli.
 
CHALAMILA ni Bichwa Komwe, Kichwa kama KOROSHO.

Japo ana point lakini kichwa chake cha kikorosho kinafanya nimpuuze.

Cc: Lamomy
 
Umaskini wa nchi hii unasababishwa na CCM, huku Chalamila akiwa mwanachama wao mtiifu, nae personally anastahili kubeba sehemu ya lawama hizo, hivyo asijigeuze mtetezi huku akiwa sehemu tatizo lilipotengenezwa na bado analikumbatia.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar, bwana Chalamila akiwa Ikulu leo amesema ukijiona una miaka 40 au zaidi na huna hela usimlaumu Rais kwani unakuwa umezaliwa wakati wa Mwalimu na katikati vimepita vipindi vingi vya uongozi, akidai kwanini alaumiwe mtu mwenye miaka mitatu kwenye uongozi.

Chalamila amesema wajibu wa Serikali ni kuandaa mazingira yatayokuwa rafiki ili kumsaidia mtu kuchemka na fursa ambazo zimeshaletwa na Serikali.

Chalamila amemaliza kwa kusema lawama ni tamko la laana linalofanya mtu ajisahau pale alipokosea na kutojisahihisha akidhani yupo alivyo kasababu ya sababu ambazo sio kweli.
Hii kauli imenichoma sana. Inauma ila ndio ukweli tutafanyaje sasa!
 
Na wale waliopata pesa kipndi cha nyuma,alafu wakaja filisika kipindi cha Mama kisa mfumuko wa bei,nao wamlaumu nani!?
 
Hoja anayo. Sasa inabidi kubadilisha mwelekeo wa lawama, Sasa wa kulaumiwa ni CCM mana tangu uhuru wao ndio wameingoza
 
Kabisa una hoja mr RC...ila tulionazo hizo hela tunataka sustainability...
Sio mara akija raisi huyu zinapuputika akija huyu zinajaa..hatutaki
 
Back
Top Bottom