PostGE2025 RC Chalamila: Vyombo vya ulinzi na usalama vimefanya kazi kubwa, bila hivyo Dar ingekuwa giza

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema miundombinu ya Mkoa huo imeendelea kudumu na kuimarika kutokana na ufanisi wa vyombo vya ulinzi na usalama, ambavyo vimefanya kazi kubwa katika kudhibiti athari za maandamano ya Oktoba 29, 2025.

Akizungumza leo Novemba 24, 2025 katika mkutano wa Dkt. Mwigulu Nchemba na wananchi wa Jimbo la Kibamba, Chalamila amesema bila juhudi hizo, madhara ya maandamano hayo yangeweza kusababisha hasara kubwa na kuathiri miundombinu mingi zaidi.

Ametoa wito kwa wazazi kuzungumza na watoto wao na kuwaelimisha kuhusu madhara ya kushiriki maandamano yenye uvunjifu wa amani.

"Tugombane tunavyoweza kugombana, lakini kamwe tusiendelee kuichoma nchi yetu wenyewe. Tukilipua nchi hii lazima na sisi tutakufa. Itakuwa ni kufanya fujo kama kukata mti wakati tuko kwenye tawi la mti huo," amesema Chalamila.
 
Vipi bado anatuambia tukawafanyie operation wake zetu wenyewe?
 
Ulituambia Dar ni salama watu wakapige kura bila wasiwasi imekuwaje tena.
 
Mpumbavu huyo....tume huru ya uchaguzi ndio dawa ya matatizo haya
 
Unaelewa chanzo cha mgogoro wa Sudan??
Nako kuna mdada wa miaka 22, mwanafunzi wa mwaka wa 2 wa Sudan University anaitwa Alaah Saalah ndiye aliyehamasisha maandamano ya kumtoa Omar Bashir mwaka 2019.

Miaka 3 baadaye Majenerali wawili; General Abdel Fattah al-Burhan wa Suda Armed Forces (SAF), na General Mohamed Hamdan Dagalo (Hemedti) wa wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) aliyekuwa kiongozi wa Janjaweed walianza kupigana mwaka 2022 na mpaka sasa watu wengi wamekufa na kupoteza makazi.
 
Nani aliyepiga marufuku na kuhujumu shughuli za vyama siasa Sudan kama ilivyofanywa hapa bongo?
Nani aliyesababisha Sudan Kusini kutengana na Sudan Kaskazini ??
 
Nani aliyepiga marufuku na kuhujumu shughuli za vyama siasa Sudan kama ilivyofanywa hapa bongo?
Nani aliyesababisha Sudan Kusini kutengana na Sudan Kaskazini ??
Waliona solution ni mapinduzi mwishowe waliopinduq na kupata madaraka wakawa ndio wale wale nchi ikawa katika sehemu mbaya zaidi
 
Waliona solution ni mapinduzi mwishowe waliopinduq na kupata madaraka wakawa ndio wale wale nchi ikawa katika sehemu mbaya zaidi
Al Bashir aliyapataje madaraka ya Urais?
Uchaguzi wake kubakia madarakani kwa miongo mitatu ulikuwa na tofauti gani na wanaoutufanyia CCM hapa bongo??
 
Al Bashir aliyapataje madaraka ya Urais?
Uchaguzi wake kubakia madarakani kwa miongo mitatu ulikuwa na tofauti gani na wanaoutufanyia CCM hapa bongo??
Akipata kwa mapinduzi akiwa kama General.

Tunaogopa fate ya Sudan unaweza kutoa worse tukaweka Worst . Si Kuna watu walisema Bora Magufuli alivyokufa ukombozi umepatikana sasa kikowapi ?

Bora anayebaki abaki tusije kujuta akaja mtu muovu zaidi yake
 
Kwa nini usifikirie fate ya Bangladesh??
 
Wakirudia tena kuleta bange zao safari hii kila nyumbu mwizi na muharibifu wa mali apigwe risasi mbele ya mali aliyoiba au kuharibu, asife tena mtu asie na hatia kisa hao nyumbu.

Hakuna huruma kwa wahalifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…