PreGE2025 RC Chalamila: Wananchi acheni kulalamika, kuna fursa nyingi kuelekea AFCON 2027 Tanzania

PreGE2025 RC Chalamila: Wananchi acheni kulalamika, kuna fursa nyingi kuelekea AFCON 2027 Tanzania

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila , amesema kuna mabadiliko ya maendeleo makubwa sana Dar Es salaam ya Miundombinu kulinganisha na Mikoa mingine. Hivyo kawataka Wafanye kazi kuliko kulalamika tuu.

Ameyasema hayo leo tarehe 10 Aprili 2025 katika Uwanja wa TP uliopo Sinza wakati wa Kusikiliza Kero za Wana wa Sinza baada ya kumaliza Ziara ya Siku mbili ya kukagua miradi ya Maendeleo Katika Wilaya Ubungo iliyoanza Tarehe 09 Aprili 2025

"Kukaa Dar es Salaam ni fursa, ukiuza maji ni Fursa, ukiuza nyanya ni Fursa. Hapa Dar es Salaam ukizubaa ukaweka malalamiko mbele utalalamika sana. Choo kikijaa utalalamika, Maji yakikata utalalamika, huu ni mji wa kufanya kazi usiku na Mchana ili kuendana na kasi ya Dar es Salaam. Unatakiwa ufike sehemu useme mimi ninaweza. Watu wanatoka Mikoani wakija Dar es Salaam wanafanikiwa lakini wewe utabaki ukisema wa hapahapa." Amesema Rc Chalamila.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Mkuu wa Dar Es Salaam amesema duniani kote kuna Tajiri na Masikini, ni jukumu lako kuchagua uwe kundi gani kwani hata china kuna Ombaomba. Amewataka Wananchi kufanya kazi kwasababu tupo kwenye ardhi imebalikiwa.

"Adui wa Maendeleo ni Kichwa chako mwenyewe". Amesema Chalamila

Chalamila amewataka Watu wenye Mtaji kuwekeza kwenye Hoteli kubwa kuelekea Mashindano ya CHAN kwani Dar Es Salaam inaenda kupokea wageni wengi sana.

"Leo tunajiandaa kwa Michezo ya CHAN na AFCON, Tanzania watakuja watu wengi hapa kuanzia 2025 hadi 2027. Sasa hivi Viwanja Vinakarabatiwa kwa pesa nyingi sana. Hapa Hoteli hazitatosha Juzi tulipata wageni Marais zaidibya 30, tulilemewa hadi tukataka wageni wengine tuwalaze Zanzibar. Wale wote waliojaliwa Mitaji waanze kujenga Mahoteli yenye Nguvu. Michezo Mikubwa inakuja, tutalaza wapi watu?" amesema Chalamila.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam amewakanya vishandu na Vibaka huku akiwaonya wananchi kuacha kujichukulia Sheria Mkononi pale wanapomkamata kibaka badala yake wawaite Polisi sababu ndio waliofundishwa jinsi ya kupambana nao.

Amewata wananchi wa Dar es salaam waendelee kukipa kodi Serikali.

Mapema asubuhi alitembelea Kituo cha Afya Makurumla, ambapo alisisitiza umuhimu wa utoaji huduma bora kwa wananchi na kusisitiza usimamizi madhubuti wa miradi ya afya.

Pia alitembelea Shule ya Msingi Ubungo Msewe, ambako aliongea na wanafunzi na walimu.
Wakati huohuo amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya Kichina ya Sichuan Road and Bridge Group (SRBG) anayefanya mradi wa upanuzi wa kipande cha Barabara ya Morogoro kutoka Ubungo hadi Kimara mwisho kwa njia njia nane kufanya kazi usiku na Mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati na mapema sana
]
IMG-20250411-WA0008.jpg
IMG-20250411-WA0006.jpg
IMG-20250411-WA0004.jpg
IMG-20250411-WA0010.jpg
 
Back
Top Bottom