Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
"Tumekuja hapa kukagua na kujiridhisha kuhusu matumizi ya fedha ambazo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amezishusha kwa ajili ya miradi ya maendeleo ili kuboresha huduma za jamii," alisema Mhe. Chongolo.
Mkandarasi alipata nyongeza ya muda kutokana na changamoto ya kusafirisha vifaa vya ujenzi. Dkt. Mwinuka alisema kuwa ujenzi huo unahusisha majengo manne, yakiwemo jengo la maabara, jengo la mionzi, jengo la kufulia, na stoo ya dawa. Hadi sasa, jumla ya shilingi milioni 583 zimetumika, na hatua za mwisho zikiendelea, ikiwa ni pamoja na uwekaji wa marumaru na kufunga milango. Kukamilika kwa hospitali hiyo kutasaidia wananchi wa maeneo ya Kata za Chitete na Msangano, na kupunguza changamoto ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya huduma za afya.