Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Godfrey Chongolo amewataka vijana wa bodaboda kujiepusha kutumiwa katika uhalifu wa mpakani hususan uvushaji wa bidhaa za magendo.
Akizungumza na kikundi cha bodaboda cha Itumba wilayani Ileje akiwa katika ziara ya siku moja wilayani humo kwa ajili ya kukagua shughuli za maendeleo, Chongolo amewataka waendesha bodaboda kuwa wazalendo na kushirikiana na vyombo vya usalama kuimarisha ulinzi hasa mipakani.