RC Chongolo: Vijana msitumie mikopo mnayopata kutoka halmashauri kulipa mahali

RC Chongolo: Vijana msitumie mikopo mnayopata kutoka halmashauri kulipa mahali

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amewataka Vijana kutotumia fedha wanazokopeshwa na Halmashauri kulipia mahari badala yake wafanyie shughuli za maendeleo akieleza kuwa Wanawake wamekuwa waaminifu kurejesha fedha hizo za asilimia 10 zinazotolewa na Halmashauri kuliko Vijana wa Kiume.

RC Chongolo amesema hayo wakati wa ziara yake katika Halmashauri za Mkoa wa Songwe za kukagua miradi ya maendeleo.

“Mikopo ile ya asilimia 10 imeanza kutolewa na Vikundi vimeshaanza kunufaika hiyo sio zawadi hiyo fedha ni fedha inayotakiwa kuzunguka na Vikundi vya wakinamama vimekuwa na uaminifu mkubwa sana tatizo kwa Vijana. Vijana wakishachukua wanaanza kufikiria miujiza, wanaanza kutafuta Mke afanye iwe sehemu ya mahari”

“Hiyo sio mahari inatakiwa ikazunguke irejeshwe ili mwingine anufaike kesho, Jiandaeni kupokea lakini jiandaeni kurejesha” amesisitiza RC Chongolo ambaye aliambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Songwe, Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda pamoja na Sekretarieti ya Mkoa katika ziara hiyo ya kukagua miradi ya maendeleo.

 
Back
Top Bottom