RC Dodoma ashauri kutoza faini ya Tsh. 10,000/- kwa wasioimba wimbo wa Taifa

Kuna mtu alipendekeza;
  1. Wimbo wa "Tazama ramani utaona nchi nzuri" ndiyo uwe wimbo wa taifa kutokana na maudhui yake
  2. Vinginevyo uliopo uondolewe maneno "wabariki viongozi wake" kwakuwa wengi wao ni wezi wakubwa
 
Tunakusaidia kwenye hili

Tatizo sio SHERIA, TATIZO ni wapi tulijikwaa vijana wakapoteza uzalendo wao!!?

Ule uzalendo ule wa kuwa tayari kuheshimu tunu za Taifa kwanini umepotea!?nani alaumiwe!?

Je nyie viongozi mnauonyesha na kuuishi huo uzalendo hadi vijana wakaiga!!?

Tukitambua hilo baas tumepona!!
 
Tatizo sio SHERIA, TATIZO ni wapi tulijikwaa vijana wakapoteza uzalendo wao!!?

Ule uzalendo ule wa kuwa tayari kuheshimu tunu za Taifa kwanini umepotea!?nani alaumiwe!?
Uzalendo ulitoweka viongozi walipoanza kuzoa mali za public na kujineemesha, kuweka wanafamilia wao kwenye nafasi za uongozi ili kulinda maslahi yao na kutetea mabaya waliyofanya nyuma
 
Mbona kama alikuwa ndotoni . Huo wimbo wa taifa unaimbwa wapi?
 
Kamwe hawawezi kujua hawajui, bali huamini wapo safarini na watafika salama.
 
Ulevi wa madaraka ni sosona mpya kwa watawala.

Wanapitia magumu, sasa wanatafuta kaupenyo hata kadoogo ka kuwabana wananchi wajue viongozi ndo wameshikilia hatma za maisha yao
 
Ni ushauri wake, lakini ni wa kipumbavu mnooo.
 
Hawa kenge huwa wanatoka wapi?wameajiliwa vipi?wanaelimu gani?badala ya kujadili matatizo ya msingi anajadili kuimba wimbo wa Taifa.
Huku mwingine anakuambia ukikutwa upo "macho juu juu"basi wewe ni kibaka!!
Nchi Haina viongozi wenye akili
 
Hivi uyu nae walimtoa wapi ,kupeka makao makuu na kumuondoa Mtaka, watu wanaiba pesa za wananchi huko yeye anakuja na ngojera eti uzalendo katika kuimba wimbo wa Taifa,
Nani ataimba wakati hajashiba? Leo Mchele kilo 3000,
 
Hakika.Uzalendo hutoka moyoni.Angalia Waingereza wanavyo simama kwenye foleni kwa zaidi ya saa 20 ili kumuaga bibi yao.
 
Hakika.Uzalendo hutoka moyoni.Angalia Waingereza wanavyo simama kwenye foleni kwa zaidi ya saa 20 ili kumuaga bibi yao.
Kweli mkuu , watu wanaona kila kinachoendelea ,watu wana uhuru wa kutoa maoni , gharama za maisha zinaendana na hali zao halisi !! Haki za binadamu zinafuatwa ! Utaacha kusimama kuaga mwili kiroho safi 😀😀😀 Halafu huku tumekazana uingereza hawana demokrasia ambayo tumesoma darasani kukaririshwa😀

Sasa mtu anatoka dukani kununua sabuni mche 4k nikute mnaimba wimbo wa taifa nitausikia kweli ? Na hela nimetoa pungufu kwenye muamala kwa ajili ya makato

Na bado wanachukua hizo Tozo lakini dharau kibao na hela hatuoni inachotusaidia zaidi ya wachache kuifaidi , uzalendo wa nini ndo maana wengine wakijichokea wanasema bora wote tukose !! Machafuko na maasi yanaanzia hapo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…