RC Halima Dedengo: Mwanafunzi ukipata mimba mshitakiwa wa kwanza unakuwa ni wewe

S
Imezoeleka katika suala la mimba mashuleni anayepewa adhabu kisheria Huwa ni mwanaume lakini kwa mkuu wa mkoa wa Singida Halima Omari Dedengo haiwi hivyo , amesema mwanafunzi wakike atakayebeba ujauzito atakuwa mshtakiwa wa kwanza na aliyempa mimba anakuwa mshtakiwa wa pili na wote watapelekwa jela.

Ameyasema hayo katika shule ya Sekondari kitaraka iliyopo halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida wakati akiwa katika ziara ya kikazi alipotembelea kuona ujenzi wa nyumba za walimu.

Aidha mkuu wa mkoa ametoa wiki moja kwa mkurugenzi kuhakikisha kunakuwa na mwalimu wa kike mmoja wa kuanzia.

Kwa upande wake Dkt. Fatuma Mganga katibu tawala mkoa wa Singida akamtaka Mkurugenzi kuhakikisha kila mwanafunzi anapewa mti wakupanda Ili kuendelea kutunza mazingira.
Sheria haipo lakini wazo lake ni zuri sanaaa. Vitoto vinajilengesha, vikipata mimba mwanaume anafungwa.
Si sawa
 
Kasome SOSPA 1998,no consent from under 18,sasa we jichanganye kisa mmekubaliana
I know of statutory rape, nilichouliza mimi ni kwanini umchukulie msichana victim ilhali karidhia? Siongelei sheria inasema nini naongela uhalisia wa jambo.

Najua kauli ya RC haina mashiko yeyote mbele ya sheria lakini haibadilishi kuwa kuna wakati hii sheria ya kumbana mwanaume tu huwa ni kandamizi.

Sikupingi chief wala kusema haupo sahihi, natofautiana mtazamo na wewe tu. Tukubaliane kutokukubaliana.

Peace.
 
Huyu RC naye hana akili kama Makonda
 
Kwa kifungu kipi kitakacho mshitaki huyo aliepewa ujauzito?
Wazo linaweza kuwa zuri ila mahakama ina taratibu zake
 
Imezoeleka katika suala la mimba mashuleni anayepewa adhabu kisheria Huwa ni mwanaume lakini kwa mkuu wa mkoa wa Singida Halima Omari Dedengo haiwi hivyo , amesema mwanafunzi wakike atakayebeba ujauzito atakuwa mshtakiwa wa kwanza na aliyempa mimba anakuwa mshtakiwa wa pili na wote watapelekwa jela.

Ameyasema hayo katika shule ya Sekondari kitaraka iliyopo halmashauri ya Itigi wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida wakati akiwa katika ziara ya kikazi alipotembelea kuona ujenzi wa nyumba za walimu.

Aidha mkuu wa mkoa ametoa wiki moja kwa mkurugenzi kuhakikisha kunakuwa na mwalimu wa kike mmoja wa kuanzia.

Kwa upande wake Dkt. Fatuma Mganga katibu tawala mkoa wa Singida akamtaka Mkurugenzi kuhakikisha kila mwanafunzi anapewa mti wakupanda Ili kuendelea kutunza mazingira.
Kwa Sheria gani ambayo itatumika kuwatia hatiani hao Wanafunzi wa kike?
Hilo litafanikiwa endapo kama Sheria zilizopo hivi sasa zitarekebishwa na kuweka kifungu hicho kitakachowatia hatiani watia na watiwa mimba.
 
I know of statutory rape, nilichouliza mimi ni kwanini umchukulie msichana victim ilhali karidhia? Siongelei sheria inasema nini naongela uhalisia wa jambo.

Najua kauli ya RC haina mashiko yeyote mbele ya sheria lakini haibadilishi kuwa kuna wakati hii sheria ya kumbana mwanaume tu huwa ni kandamizi.

Sikupingi chief wala kusema haupo sahihi, natofautiana mtazamo na wewe tu. Tukubaliane kutokukubaliana.

Peace.
Ofcoz hii sheria ilitungwa kwa jazba sana labda kutokana na nature ya kosa na impact yake kwa jamii.
 
Kama ingekua hivyo tatizo la mimba za shuleni lingeisha, itakua vizuri Sana kama hiyo itakua Sheria rasmi anaepaswa kupona ni yule aliebakwa tuu
 
Yuko sahihi kwa asilimia 100.
Lazima msichana ajilinde mwenyewe kwanza kimsingi(ajengewe fikra za kujilinda), sheria na jamii kwa ujumla ni hatua ya pili.
Wasichana hujiachia kwa sababu hawajui wajibu wao kujilinda na pia madhara wayapatayo.
 
Kwa hiyo anamaanisha aliyekula na aliyeliwa wote wana makosa?!😃
 
Hana akili kivipi labda ,we unadhani hivi vibint vya sasa kuna kinacho bakwa? Hata kama kina miaka 24?
Kuna fact nyingi za kusababisha mimba, umasikini, mila na desturi, umbali wa kutoka nyumbani kwenda shule n.k, wao wanatakiwa kutengeneza miundombinu ya shule wanafunzi wabaki shuleni na siyo kutembea kwa miguu 20km kwenda na kurudi na huku akitegemea lift kutoka kwa bodaboda.
 
Kwa hofu ya kunyea debe tutarajie cases za Utoaji mimba kuongezeka tena vichochoroni hivyo vifo pia havitakosekana.

Kubeba,watabeba tu hata watishiwe maisha.
 
Kuna fact nyingi za kusababisha mimba, umasikini, mila na desturi, umbali wa kutoka nyumbani kwenda shule n.k, wao wanatakiwa kutengeneza miundombinu ya shule wanafunzi wabaki shuleni na siyo kutembea kwa miguu 20km kwenda na kurudi na huku akitegemea lift kutoka kwa bodaboda.
Umbali ni sababu nyepesi, sana na impact yake ni ndogo sana tatizo kubwa ni mmomonyoko wa maadili uliopo kwa wazazi na utandawazi ulio shindikana kudhibitika tanzania l, watoto wako huru kuanza umalaya wangali wadogo na wapo huru
 
Back
Top Bottom