RC Homera wa Mbeya amejiuzia gari la Serikali kinyemela?

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,132
Reaction score
64,416
IMG-20250618-WA0009.jpg
Screenshot_20250618_103333_Word.jpg

Utata gari la RC

MKUU mmoja wa mikoa nchini (majina yanahifadhiwa kwa sasa), anadaiwa kuingia katika kashifa ya kununua gari la Serikali (Shangingi), alililokuwa akilitumia awali, Raia Mwema imebaini.

Uchunguzi wa Gazeti hili, umebaini kuwa Mkuu huyo anadaiwa kutumia madaraka yake kufanikisha ununuzi wa gari hilo ambalo sasa ni mali yake binafsi.

Juzi alipopigiwa simu kuzungumzia madai hayo, kwa siku mbili mfululizo Mkuu huyo hakuwa tayari kusema chochote na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.

Jana kiongozi huyo alipigia simu na aliposikia utambulisho wa mwandishi, aliomba kurejea muda mfupi baadaye, akidai kupokea simu nyingine muhimu zaidi kwake wakati huo kuipokea.

Baada ya hapo hakurejea tena.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, gari hilo la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser GXR, namba za 6201, lilikuwa likitumiwa na Mkuu wa Mkoa huyo hadi mwaka jana.

"Mwaka jana ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ilipokea gari jipya kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa. Hali hiyo ilimfanya aanze figisu kutaka anunue gari hilo la awali na kufanikiwa," alisema mtoa taarifa wetu. Taarifa zaidi zinadai kuwa baada ya Serikali kuleta gari jipya, alianza kutengeneza mazingira ya kuhakikisha gari alilokuwa akitumia mwanzo, halitumiki tena kwa shughuli za Serikali tangu lilipokuja jipya.

Taarifa zaidi zinadai kuwa Agosti mwaka jana wakati wa mbio za Mwenge, alikuwa likizo na nafasi yake aliikaimisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

"Hivyo Kamati ya Mwenge Mkoa wa Mbeya, ilitumia gari hilo kubeba kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa kipindi chote cha ukiwa mkoani hapa," alisema mtoa taarifa wetu.

Aliongeza, kuwa baada ya kupata taarifa kuwa gari hilo linatumika kwa shughuli za Mwenge, alikuwa 'mbogo' na kuagiza lisitumike tena na badala yake liegeshwe kwenye maegesho ya ofisi yake.

"Aliagiza liazimwe gari kutoka taasisi nyingine litumike kwa shughuli hizo. Hata hivyo lililoazimwa, ilipata hitilafu ikabidi gari lake liendelee kutumika," alisema.

Ilielezwa kuwa lengo la kuzuia gari hilo kutumika tena, ni kwa sababu alikuwa na mpango wa kulinunua na aliutekeleza mwaka huu na mpaka sasa gari hiyo ni mali yake.

Uchunguzi umebaini kuwa gari hilo lilikuwa bado jipya, hivyo lingeendelea kutumika kwa shughuli za Serikali.

"Mfano, mpaka sasa Mkuu wa Wilaya hana gari, anatumia la Idara ya Elimu Sekondari, hivyo ingefaa gari hilo apewe, ili kuepusha Serikali kuingia gharama ya kununua gari kwa ajili ya mkuu huyo wa wilaya wakati la Serikali lipo lakini sasa ni mali ya mtu binafsi," alisema. Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Mkuu wa Mkoa huyo alifuata taratibu zote za manunuzi za mali za Serikali.

Kwa mujibu wa taratibu hizo ni kwamba taarifa ya kwanza inapaswa kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa (RAS) ambaye naye anapeleka taarifa hizo kwa Katibu Mkuu (TAMISEMI) "Maombi hayo yakishafika TAMISEMI, nao wanapekeka kwa Wizara ya Uchukuzi kwa Katibu Mkuu. Hao ndio wenye mali zao na kazi yao ni kufanya uhakiki wa thamani wa gari inayotaka kuuzwa," alisema mtoa taarifa wetu na kuongeza kuwa.

"Hatua nyingine ni kufikisha maombi hayo kwa Katibu Mkuu Hazina ambao ndio wanatoa kibali sasa cha mauzo hayo," alisisitiza Mtoa taarifa wetu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema Mkuu wa Mkoa huyo alifuata hatua zote na kwamba sio mtumishi wa kwanza kununua gari au mali zingine zozote za Serikali.

Alisema hata miaka ya nyuma baadhi ya watumishi wa umma waliuziwa nyumba kwa utaratibu uliowekwa na Serikali na mambo mengine yanayo endelea ni mambo ya siasa za uchaguzi.
 
Unajisumbua Mama amesema nyie mnaotoa siri acheni kiherehere watu wale kwa ukubwa /urefu wa kamba zao.Wewe chukua mradi usiwe kinyume na CCM tu unaruhusiwa kuvunja sheria
 
View attachment 3374327View attachment 3374328

Wengi tuu wanajiuzia ,hizo gari zinakuwa zimeisha km zinazotakiwa na Serikali ila kimtaa mtaa Bado ni mpyaaaaa.
 
Hii nchi inahitaji mabadiliko ya haraka sana ya kimfumo. Sasa gari ni zina! Kwa nini auziwe Mkuu wa Mkoa? Kwa nini lisitumike jwa shughuli nyingine? Na kama kulikuwa kuna ulazima wa kuliuza; kwa nini kusiwepo na mnada wa wazi ili wanunuzi washindanishwe?

Yaani watu wanalipa kodi kwa vitisho, halafu hela zao mnaenda kuzichezea kwa kununulia magari ya kifahari, na baada ya muda mfupi mnajiuzia tena nyinyi wenyewe!! Hili jambo halikubaliki hata kidogo.
 
Serikali iwe serious kidogo CAG alishauri mara nyingi tu kwamba mali za serikali ambazo ni chakavu au hazitumiki tena ziuzwe kwa mnada wa hadhara ili kupata value for money
 
Taarifa imemficha muhusika
Wakati kichwa kimemtaja Homera.
Ni Nini hiki!?
 
Huyu ni vita kawawa na dada yake zamarad kawawa,kifupi hii familia Ina haha baada ya kuona Wenye Namtumbo Yao Sasa wame amua kuikombi kutoka kwenye familia ya muasisi.
Kama familia hii ungekuwa Ina sikia ushauri wange kaa mbali na Jimbo la Namtumbo wake elekeza nguvu zao kwenye biashra zao walizo zipata kupitia Jimbo hili!!
 
Sasa hebu fikiria, unakutana na habari kubwa, ya moto, imeanza na maneno mazito ‘MWANDISHI WETU’ halafu ukisubiri mwandishi atajwe — kimya! Hapana bwana, hii sio breaking news, hii ni breaking trust. Hii ni kama kupika wali wa nazi halafu hakuna nazi, wala chumvi — unapigwa tu harufu na maneno matupu.

Kama habari ni ya kweli, si useme tu kwa majigambo kama ‘Ndio! Hii nimeifuatilia mimi fulani, kwa jina hili, kwenye chanzo hiki!’ Mbona unapiga picha ya ugali lakini unaficha sahani? Mbona unalipua habari lakini unavaa mask? Hii ni dalili ya ama kuandika habari haramu au kupika propaganda za kificho.

Na kwa hilo, mi sitaki kushiriki. Siungi mkono habari za kubahatisha ambazo hata mwandishi mwenyewe anajificha kama kahama na deni. Kama huwezi simama na ukweli wako kwa uwazi, basi hiyo si habari — ni hadithi ya jioni.
 
View attachment 3374327View attachment 3374328
Utata gari la RC

MKUU mmoja wa mikoa nchini (majina yanahifadhiwa kwa sasa), anadaiwa kuingia katika kashifa ya kununua gari la Serikali (Shangingi), alililokuwa akilitumia awali, Raia Mwema imebaini.

Uchunguzi wa Gazeti hili, umebaini kuwa Mkuu huyo anadaiwa kutumia madaraka yake kufanikisha ununuzi wa gari hilo ambalo sasa ni mali yake binafsi.

Juzi alipopigiwa simu kuzungumzia madai hayo, kwa siku mbili mfululizo Mkuu huyo hakuwa tayari kusema chochote na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno, hakujibu.

Jana kiongozi huyo alipigia simu na aliposikia utambulisho wa mwandishi, aliomba kurejea muda mfupi baadaye, akidai kupokea simu nyingine muhimu zaidi kwake wakati huo kuipokea.

Baada ya hapo hakurejea tena.

Kwa mujibu wa uchunguzi wetu, gari hilo la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser GXR, namba za 6201, lilikuwa likitumiwa na Mkuu wa Mkoa huyo hadi mwaka jana.

"Mwaka jana ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ilipokea gari jipya kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa. Hali hiyo ilimfanya aanze figisu kutaka anunue gari hilo la awali na kufanikiwa," alisema mtoa taarifa wetu. Taarifa zaidi zinadai kuwa baada ya Serikali kuleta gari jipya, alianza kutengeneza mazingira ya kuhakikisha gari alilokuwa akitumia mwanzo, halitumiki tena kwa shughuli za Serikali tangu lilipokuja jipya.

Taarifa zaidi zinadai kuwa Agosti mwaka jana wakati wa mbio za Mwenge, alikuwa likizo na nafasi yake aliikaimisha kwa Katibu Tawala wa Mkoa.

"Hivyo Kamati ya Mwenge Mkoa wa Mbeya, ilitumia gari hilo kubeba kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa kipindi chote cha ukiwa mkoani hapa," alisema mtoa taarifa wetu.

Aliongeza, kuwa baada ya kupata taarifa kuwa gari hilo linatumika kwa shughuli za Mwenge, alikuwa 'mbogo' na kuagiza lisitumike tena na badala yake liegeshwe kwenye maegesho ya ofisi yake.

"Aliagiza liazimwe gari kutoka taasisi nyingine litumike kwa shughuli hizo. Hata hivyo lililoazimwa, ilipata hitilafu ikabidi gari lake liendelee kutumika," alisema.

Ilielezwa kuwa lengo la kuzuia gari hilo kutumika tena, ni kwa sababu alikuwa na mpango wa kulinunua na aliutekeleza mwaka huu na mpaka sasa gari hiyo ni mali yake.

Uchunguzi umebaini kuwa gari hilo lilikuwa bado jipya, hivyo lingeendelea kutumika kwa shughuli za Serikali.

"Mfano, mpaka sasa Mkuu wa Wilaya hana gari, anatumia la Idara ya Elimu Sekondari, hivyo ingefaa gari hilo apewe, ili kuepusha Serikali kuingia gharama ya kununua gari kwa ajili ya mkuu huyo wa wilaya wakati la Serikali lipo lakini sasa ni mali ya mtu binafsi," alisema. Hata hivyo taarifa zinaeleza kuwa Mkuu wa Mkoa huyo alifuata taratibu zote za manunuzi za mali za Serikali.

Kwa mujibu wa taratibu hizo ni kwamba taarifa ya kwanza inapaswa kutoka kwa Katibu Tawala Mkoa (RAS) ambaye naye anapeleka taarifa hizo kwa Katibu Mkuu (TAMISEMI) "Maombi hayo yakishafika TAMISEMI, nao wanapekeka kwa Wizara ya Uchukuzi kwa Katibu Mkuu. Hao ndio wenye mali zao na kazi yao ni kufanya uhakiki wa thamani wa gari inayotaka kuuzwa," alisema mtoa taarifa wetu na kuongeza kuwa.

"Hatua nyingine ni kufikisha maombi hayo kwa Katibu Mkuu Hazina ambao ndio wanatoa kibali sasa cha mauzo hayo," alisisitiza Mtoa taarifa wetu ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema Mkuu wa Mkoa huyo alifuata hatua zote na kwamba sio mtumishi wa kwanza kununua gari au mali zingine zozote za Serikali.

Alisema hata miaka ya nyuma baadhi ya watumishi wa umma waliuziwa nyumba kwa utaratibu uliowekwa na Serikali na mambo mengine yanayo endelea ni mambo ya siasa za uchaguzi.
Vidomodomo wakamatwe wafunguliwe kesi za ugaidi wanyongwe hadi wafe ili tuishi kwa amani.
 
Yaan kipi Cha kushangaa hapo Kama gari kanunua yeye na la kwake ,munaandika vitu vya ajabu ili kumchafua mtu lakin kila mtu Ana mipaka yake au mumetumwa na mtu ili kumchafua mkuu wa mkoa wa mbeya
 
Back
Top Bottom