Pre GE2025 RC Iringa ahimiza wananchi kushiriki kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura

Pre GE2025 RC Iringa ahimiza wananchi kushiriki kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Kheri James amewataka wananchi wilayani humo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kutekeleza haki yao ya Kikatiba kuchagua viongozi wanaotaka kuwaongoza katika jamii.

Pia, Soma: Katibu Mwenezi CCM Iringa awahimiza wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura

Akizungumza na Waandishi wa habari jana Disemba 26, 2024 ofisini kwake Kheri James amebainisha kuwa zoezi hilo litaanza leo tarehe 27 Disemba 2024 hadi tarehe 2 Januari 2025 kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni na maandalizi yote yamekamilika.

Aidha Kheri James amewaomba viongozi wa dini na kimila kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao ili kuweza kushiriki vyema uchaguzi mkuu ujao.
 
Back
Top Bottom