Wakuu,
Lazima utafute namna ya kumsifia mama, la sivyo ugali utakata!
===
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, amewataka wananchi kuendelea kumuombea na kumuunga mkono Rais Samia ili aendelee kitimiza maono ya kusogeza huduma bora za kijamii kwa wanakatavi na watanzania kwa ujumla.
Mrindoko Ameyasema hayo katika hafla ya iftari ambayo iliandaliwa na ofisi yake na kuwakutanisha waumini wa dini zote na kusisitiza upendo, amani, utulivu na Ushirikiano ili kuufanya mkoa wa Katavi tuendelee kusongambele kimaendeleo.
Nae Kaimu Shekh Mkuu wa mkoa wa Katavi amewataka waumini kuendelea kulinda amani hasa kipindi hiki cha uchaguzi huku baadhi ya washiriki wakimshukuru Mkuu wa mkoa kwa kuendelea kuwa kiunganishi cha dini zote ndani ya mkoa wa Katavi.