RC Katavi asema "Mkurugenzi asipotekeleza agizo la usafi Stendi ya Mizengo Pinda nitaona cha kufanya"

RC Katavi asema "Mkurugenzi asipotekeleza agizo la usafi Stendi ya Mizengo Pinda nitaona cha kufanya"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Baada ya Member wa JamiiForums.com kutoa andiko Julai 16, 2025 akielezea changamoto za uchafu iliyopo kwenye Stendi Kuu ya Mabasi ya Mizengo Pinda hasa upande wa Vyoo vya Wanaume ambavyo vilionekana kujaa, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Hoza Mrindoko amefika katika stendi hiyo na kueleza kuwa alitoa maelekezo ya usafi kwa Mkurugenzi lakini hayajatekelezwa.

RC Mwanamvua amefanya ziara katika Stendi Kuu ya Mabus Mizengo Pinda kujionea hali ilivyo ambapo amesema anasubiri siku saba alizotoa ili usafi ufanyike kisha atajua cha kufanya.

Pia ametoa wito wa watu kuwa na matumizi mazuri ya vyoo na miundombinu mingine ambayo ni ya umma kwa kuwa dhana ya matumizi imekuwa siyo nzuri hasa katika miundombinu ya umma.

Hoja ya Mdau kuhusu vyoo hivyo ipo hapa ~ Natamani Viongozi wa Wilaya na Mkoa Katavi wangekuwa wanatumia Vyoo vya Stendi ya Mizengo Pinda labda wangevijali

Pia soma ~ Halmashauri ya Mpanda yafafanua uchafu Vyoo Stendi ya Mizengo Pinda, yasema inafanya ukarabati
Screenshot 2025-07-16 124030.jpg

Hali ya vyoo ilivyo​
 
Back
Top Bottom