PreGE2025 RC Kihongosi: Hatuitaji vurugu Simiyu, wazazi waambieni vijana wenu

PreGE2025 RC Kihongosi: Hatuitaji vurugu Simiyu, wazazi waambieni vijana wenu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Kenani Laban Kihongosi amewataka Wazazi Mkoani humo kuwaepusha na kuwakanya Vijana wao kujiepusha na wanasiasa wanaotaka kuwatumia kuvuruga na kuharibu amani ya Tanzania hususani ya Mkoani Simiyu, akisisitiza umuhimu wa amani kwa maendeleo ya Mkoa wa Simiyu.

1746428543645.jpeg
Kihongosi amebainisha hayo leo Jumapili Mei 04, 2025, wakati akizungumza na wanachama na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Bariadi, akisisitiza kuchukua tahadhari dhidi ya chokochoko za kisiasa ambazo zimeibuka katika mwaka huu wa Uchaguzi Mkuu wa Kuwachagua madiwani, Wabunge na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

"Mwaka huu kuna watu wameamua kwa makusudi kabisa kuleta vurugu, Mimi niombe na niseme waambieni watoto na ndugu zenu kwamba wana wajibu mkubwa wa kulinda amani.

"Kuna watu wanaohamasisha watu waende kwenye maandamano naamini mnawajua, kuna watu wanawaambia watu msishiriki uchaguzi, naamini mnawajua, kuna watu wanawaambia mpambane na serikali, naamini mnawajua. Sasa tuulizane hapa kuna mtu anaweza kupambana na serikali? Anayekutuma ukuafanya vurugu huwezi kumuona yeye, Mkewe wala familia yake ikipata madhara."
 
ccm huwa wanatafuta tafuta watu waliosoma kwa kuunga unga km huyu kuwatumia kupiga mikwala ya kitoto km hivi alivyosema..awaambie hao anaongea nao wengine aachane nao kabisa, tenda haki, acha kutisha watu..! watu hawandamani kwa kupenda, wanaandamana kupinga uovu mbona hayo hayasemi..?
 
Back
Top Bottom