Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Dkt Anna Mghwira ametangaza kukutwa na maambukizi ya virusi vya Corona baada ya kufanyiwa vipimo siku tatu zilizopita.
Mama Mghwira anasema kuwa hajui amepata wapi na lini maambukizi hayo. Lakini amesema kuwa hana dalili zozote na aliamua tu kupima kujua afya yake.
--
Mama huyu jasiri ni mfano wa kuigwa na viongozi wote Tanzania hasa wakati huu wa korona. Ameonesha njia, ujasiri, uwazi na anatoa ushauri mzuri sana, baadhi;
Asante sana mwanamke shujaa, umeonesha njia. Wale wanaosema "amepata matatizo ya kupumua" acheni ushamba na ujinga.
- Amekuwa na corona bila kujua
- Watu wanapaswa kupima hata kabla ya kuwa na dalili hii husaidia kuwahi virusi kabla havijaingia kwenye mapafu
- Korona sio jambo la kuonea aibu na kuficha, tuwe wawazi na ili tupate matibabu mapema
- Hakuna haja ya kuwa na hofu, cha muhimu ni kuchukua hatua stahiki
Waziri Mkuu wa Uingereza alisema waziwazi kwamba amepata corona. Mwana mfalme wa Uingereza (Prince Charles) alisema waziwazi kwamba ameugua corona. Binti mfalme wa Hispania aliugua corona na kufariki na ikatangazwa waziwazi kwamba ni corona.
Jamani sisi watanzania tunaficha corona na kuona aibu kutaja ili iweje? Huu ndio ujinga wa Africa na ndio maana magonjwa yanatumaliza sana.