RC Kunenge: Anayejiona hawezi kwenda na kasi ya Serikali hii atupishe, akae pembeni. Watendaji mnajivuta mno

RC Kunenge: Anayejiona hawezi kwenda na kasi ya Serikali hii atupishe, akae pembeni. Watendaji mnajivuta mno

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,618
Reaction score
9,611
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amewataka Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi, Wastahiki Meya, Makatibu Tawala na Wakuu wa Idara kuhakikisha wanasimamia kikamilifu majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha miradi yote yenye kutatua kero za wananchi inakamilika.

RC Kunenge ametoa agizo hilo wakati wa ziara ya kukagua miradi Wilaya ya Kinondoni ambapo akiwa kwenye kiwanda Cha kuchakata mbolea itokanayo na taka zinazozalishwa Jijini humo kilichopo Mabwepande RC Kunenge ameelekeza Manispaa ya Kinondoni kuwaondoa wote waliovamia na kujenga kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 14.

Aidha RC Kunenge ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha Kiwanda hicho kinaanza kufanya kazi kabla ya Mwezi February mwakani ambapo ameeleza kuwa uwezo wa Kiwanda utakuwa ni kuchakata tani 50 za taka na kupata tani 30 za mbolea kwa siku.

​
 
Unadhani uongozi ni kufokafoka, kutukana watu ama kukunja ndita?

Au unadhani uongozi ni kuita media na kutafuta kiki?

Kunenge bonge la kiongozi kwa taarifa yako.
 
Akimalizana na hao wanaotapisha majitaka Kinondoni, aende Kawe nyuma ya Maringo kuelekea Baobao Apartments, watu wamejiunganishia mabomba ya majitaka kuelekea mfereji wa maji.
 
Hivi hii serik ina kasi gani? Hakuna serikali iliyojaa uzembe kama hii.

Wanaweza tu matamko.
 
Kabla hujajisifu unambio, msifu na anae kukimbika.. kabla ya kuwa RC alikuwa Mkurugenzi.. kwa mambo yalivyo inaonekana kabisa Makonda alikuwa anambeba sana
 
Back
Top Bottom