Uchaguzi 2020 RC Kunenge awahakikishia wananchi usalama siku ya Uchaguzi, asema atakayefanya fujo kukiona cha moto

Uchaguzi 2020 RC Kunenge awahakikishia wananchi usalama siku ya Uchaguzi, asema atakayefanya fujo kukiona cha moto

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya fujo siku ya uchaguzi ambapo ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama.

RC Kunenge ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ambapo ametoa wito kwa wananchi wote waliojiandikisha kutumia haki yao ya msingi kwa kutijokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha RC Kunenge ameeleza kuwa hali ya amani na utulivu kwenye jiji hilo ni shwari na utaendelea kuwa shwari siku zote hivyo hakuna sababu yoyote ya wananchi kuwa na wasiwasi.

Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa ngazi ya Urais, Wabunge na Madiwani utafanyika October 28 ambapo Rais Dkt. John Magufuli amepanga siku hiyo kuwa ya mapumziko ili kila Mwananchi aweze kupata nafasi ya kutumia haki yake ya msingi ya kupiga kura.

1603365786973.png

Attachments

Amani ipo na itakuwepo siku zote, hicho ni kipawambele cha Ccm

Kama mnadhani amani haipo fanya vurugu km sera ya Chadema inavyotaka
Suala la AMANI ni kuliombea Mungu siyo porojo za mdomoni, kama HAKI haitotamalaki basi moto utawaka.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya fujo siku ya uchaguzi ambapo ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama.

RC Kunenge ametoa onyo hilo wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari ambapo ametoa wito kwa wananchi wote waliojiandikisha kutumia haki yao ya msingi kwa kutijokeza kwa wingi kwenye vituo vya kupigia kura ili waweze kuchagua viongozi wanaowataka.

Aidha RC Kunenge ameeleza kuwa hali ya amani na utulivu kwenye jiji hilo ni shwari na utaendelea kuwa shwari siku zote hivyo hakuna sababu yoyote ya wananchi kuwa na wasiwasi.

Uchaguzi Mkuu wa viongozi wa ngazi ya Urais, Wabunge na Madiwani utafanyika October 28 ambapo Rais Dkt. John Magufuli amepanga siku hiyo kuwa ya mapumziko ili kila Mwananchi aweze kupata nafasi ya kutumia haki yake ya msingi ya kupiga kura.

Wananchi ni wengi mara 200 ya Polisiccm na kukiwa na haki Polisiccm huonekana ni wengi mno lakini kusipo na haki Polisiccm wataonekana wachache mno, angalia kule Nigeria sasa nguvu ya umma imewalemea polisi
 
Wee iba kura then uone kitakachotokea pamoja hapo mapolice wako watano.
 
Wee iba kura then uone kitakachotokea pamoja hapo mapolice wako watano.
Polisiccm ni wachache sana endapo wananchi wakiamua kukomaa wakaanza kudai haki
 
Suala la AMANI ni kuliombea Mungu siyo porojo za mdomoni, kama HAKI haitotamalaki basi moto utawaka.
Ya Malawi Zambia kenya congo Ghana Gambia yanaenda kutokea na Nchi itapata uhuru tarehe 28 toka kwa Mkoloni mweusi kaburu tokea chato
 
Maji yaliyotulia yana kina kirefu
CCM bila uchakachuaji bila wizi wa kura bila Polisiccm bila Tumeccm bila mahakamaccm bila wakurugenziccm bila Msajiliccm ni weupe sana hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu ataipigia CCM kura
 
Ndo nani uyu .mjinga mjinga
Rudia kusoma na ufuate taratibu na sheria za uchaguzi

"Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge ametoa onyo kali kwa watu au vikundi vya watu vilivyopanga kufanya fujo siku ya uchaguzi ambapo ameeleza kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na usalama."

Uwashauri na wenzio☺
 
Nchi ina miaka 59 hakuna maendeleo licha ya kuwa na rasilimali nyingi kuliko mataifa mengi Duniani, CCM wamechukua pesa za viwanda za walipa kodi za maendeleo na kuzitumia kwenye mambo yasiyo na tija kwa Taifa ikiwemo kudidimiza demokrasia kuwabambikia kesi kesi kuwapiga risasi uonevu unyanyasaji mwingi na mengineyo mengi ya hovyo ni vigumu Nchi kupata maendeleo endapo inaendelea kutawaliwa na CCM yenye watu wapenda visasi wapenda kuwakomoa wafanyabiashara kuwabambikia kodi TRA kuwafirisi mali zao kuwapa kesi za uhujumu uchumi na uovu kibao .
 
Back
Top Bottom