Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Kunenge alitoa agizo hilo katika mkutano wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Pwani uliofanyika Kibaha, ukiwahusisha wadau wa maendeleo na wataalamu wa sekta hiyo.
Alisisitiza umuhimu wa kuwa na mpango wa utekelezaji wa ujenzi wa barabara, hasa zile zilizokuwa sehemu ya ahadi za uchaguzi. Pia, alihimiza tathmini ya barabara zilizokamilika, zinazoendelea, na zile ambazo hazijaanza, huku kipaumbele kikiwekwa kwenye barabara muhimu zaidi.
"Tunapaswa kutambua ni barabara zipi zimekamilika, zipi bado na zipi hazijaanza. Waheshimiwa wabunge wanapaswa kutueleza barabara chache zenye umuhimu wa kipekee ili zipewe kipaumbele, hata kama ni tano au kumi, ni lazima tujue zipi tunapaswa kuzitekeleza haraka ili kuepuka msukosuko kwa serikali na chama.
Aliendelea kueleza kuwa utekelezaji wa miradi hiyo unapaswa kuzingatia maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Alisisitiza kuwa barabara zenye mchango mkubwa kwa uchumi zinapaswa kupewa kipaumbele, huku serikali ikiepuka miradi inayoweza kuwa mzigo mkubwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, alieleza kuwa miundombinu ya barabara ni changamoto kubwa Kisarawe kutokana na milima mingi na bajeti ndogo. Alisema wananchi wanalia kuhusu hali mbaya ya barabara, jambo linalohatarisha nafasi za viongozi katika uchaguzi ujao.
"Tunaelekea kipindi cha mvua na pia kampeni zinakaribia. Kila mkutano ninaofanya, asilimia kubwa ya maswali ni malalamiko ya wananchi kuhusu barabara. Wilaya yetu ina historia ya zaidi ya miaka themanini, lakini tuna kilomita saba pekee za lami. Hali hii inafanya kuwa changamoto kubwa kwa wabunge na madiwani wetu katika uchaguzi ujao,"
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025