Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mvua yaacha vilio Dar
WATU 13 wamefariki dunia, wakiwamo wanane ambao vifo vyao vimetokana na mvua kubwa iliyonyesha juzi jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi, watu watano ambao ni wa familia moja wamefariki dunia baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuungua moto.
Akizungumza na Nipashe jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Janet Magomi, alisema vifo vilivyotokana na mvua vimetokea Mto Msimbazi.
Alisema kwamba, Mto Msimbazi eneo la Kariakoo kulikutwa miili ya watu watano ambayo imehifadhiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kati yake, mitatu tayari imeshatambuliwa na ndugu zao.
“Maeneo ya Buguruni, kuna taarifa ya watu wengine wawili, mwanaume na mwanamke ambao miili yao iliokotwa kwenye mto na maeneo ya Ukonga ipo taarifa ya mtu mmoja aliyeokotwa Mto Mvule, miili yote ipo Muhimbili,” alisema.
Kamanda Magomi alisema kati ya watu hao waliofariki dunia kutokana na mvua hizo za juzi, watoto ni wawili.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, watoto hao walifariki dunia wakati wakisaidiana kuokoana kwenye Mto Msimbazi.
Kuhusu tukio la moto, Kamanda Magomi alisema lilitokea juzi saa nne usiku Kata ya Pugu, Tarafa ya Ukonga wilayani Ilala jijini.
“Kuna nyumba iliungua na wamefariki wanafamilia watano ambao ni mke, watoto watatu na wifi ambaye ni mdogo wa mume wa mke aliyefariki dunia,” alisema.
Kamanda Magomi alisema watu hao walifariki dunia baada ya kufikishwa hospitalini.
“Walikuwa hawana majeraha wakati wakipelekwa hospitali, lakini wakati wakitaka kupatiwa matibabu, walionekana wameshafariki dunia, chanzo cha moto huu tunaendelea kuchunguza ila mashuhuda wanasema ulianzia sebuleni," alisema.
Aliongeza kuwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo hilo la tukio na kuuzima ili usiendelee kuleta madhara zaidi.