JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Amos Makalla amesisitiza umuhimu wa kutengeneza miundombinu ya njia kwenye masoko inayoweza kusaidia kukabiliana na majanga ya moto huku akisema amechoka kusikia ajali za moto katika mkoa huo.
Kauli hiyo ameitoa jana Februari 13, 2022, wakati anatoa pole kwa wafanyabishara wa Soko la Mbagala Rangi Tatu lililoungua kwa moto ulioanza kuwaka kuanzia saa 10:00 alfajiri ya kuamkia jana muda sawa na bweni la wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Ilala Islamic lilipoanza kuungua.
Katika matukio hayo yote mawili yaliyotokea alfajiri hiyo ya kuamkia leo hakuna madhara kwa binadamu baada ya Jeshi la Zimamoto na uokoaji kuwahi na maeneo ya matukio na kuzima moto ambao hata hivyo umesababisha hasara kwa baadhi ya vitu kuteketea kwa moto.
Makalla amesema amechoka kusikia ajali za moto katika Mkoa wa Dar es Salaam kwani sababu zinazotolewa kuhusiana na matukio mengi zinafanana huku akiwataka viongozi wa masoko kushirikiana na wafanyabishara kuimarisha ulinzi.
"Kupitia masoko naomba wafanyabisha kwa kushirikiana na viongozi wenu kujijengea tabia ya kuimarisha ulinzi wenyewe kwani unaanzia kwenu, mimi nimechoka kusikia ajali za moto, wekeni miundombinu ya njia zinazopitika ili iwe rahisi kukabiliana na ajali kama hizi zinapotokea," amesema Makalla.