RC Makalla atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono, awataka Polisi kuvaa kiraia na kujifanya wateja

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
makalla-12-1080x570-1.jpeg

Picha: Mkuu wa Mkoa Amos Makalla

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa Wiki moja kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanadhibiti watu wote wanaofanya biashara ya Ngono kwenye eneo la Manzese Uwanja wa Fisi baada ya suala hilo kulalamikiwa na Wananchi.

Malalamiko hayo yametolewa wakati wa Mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua Migogoro ya Wananchi Jimbo la Kinondoni ambapo wamedai kuwa imefikia hatua biashara hiyo inahusha pia utumikishaji wa kingono kwa watoto wadogo Jambo ambalo ni kinyume na sheria na maadili.

Kutokana na hilo RC Makalla amewaelekeza Jeshi la Polisi kuwatuma askari watakaovaa nguo za Kiraia na kuwanasa watu wote wanaofanya biashara ya ngono.

Aidha RC Makalla ameelekeza Viongozi wa kata na Mtaa huo kuhakikisha wanatoa ushirikiano wa kutosha kumaliza suala hilo.

Bongo Five
 
Dalili za kukosa ubunifu na kukosa kazi za kufanya.

Hii biashara imekuwapo hata kabla ya nabii Issa.

Hii biashara iko duniani kote na katika miji yote.

Wewe kama si mteja au mdau inakuhusu nini?

Hivi wa machinga kesha malizana nao?
 
Back
Top Bottom