RC Makalla atoa Wiki moja kukomeshwa biashara ya ngono, awataka Polisi kuvaa kiraia na kujifanya wateja

Huo ndio mgogoro wa maana alioupa uzito. Unashindana na biashara ya ngono, utaondoka kwenye hiyo nafasi, ukiiacha biashara iko pale pale.
 
Safi sana.Biashara ya ngono inadhalilisha utu, Ndoa haziheshimiwi tena sababu ngono imekua rahisi sana.wanandoa wakitofautiana kidogo mmoja wao anaenda kununua ngono badala ya kufanya suluhu ndani ya nyumba.
[emoji3525]
 
Aangalie hapo polisi wake wasije kubakwa wao.
Maana watakula papuchi kwenye malipo watataka kitonga watoe kitambulisho ndio kubakwa kwao kutaanzia hapo.
 
Nchi za wenzetu iko formalized na wanalipa kodi, pia wana maeneo maalum siyo kuzurura zurura kama kuku wa kienyeji......kama hao makahaba hawawezi kuacha ni fursa sasa kwa serikali kuweka regulations na pia kutoza kodi au ushuru ili kiwe chanzo mojawapo cha mapato tuongeze madarasa mengine 200.....
 
Kubwa hii biashara irasimishwe tu wawekwe kwenye mnyororo wa thamani rasmi..
 
Biashara ya ukahaba haiwezi kumalizwa kwa Amri na matamko ya viongozi. Hapa Makala anajifurahisha tu. Hao Polisi wengi wao Ni wateja wazuri na zaidi huwa wanahitaji huduma kwa vitisho.
 
Hivi huyu RC ana elimu gani? Open University au zile Executive degree za MU?! Kikwetu makala maana yake Mkaa.
 
Arudi vitabuni kwanza akajue History ya hio biashara kongwe kabisa
 
Waheshimiwa wenyewe ndio wateja wakubwa wa dada poa
 
RC ajikite kwenye mambo ya msingi
Hii biashara ipo toka enzi za Yesu haijawahi Kufa na haitakufa tusipoteze resources bure
Nashindwa kuelewa, yani Amina ameamua kumuuzia Jose uchi wake, sasa Mimi kinaniuma nini? Nyuchi zinazotumika hapo ni zangu?
 
Ndiyo maana wengi hawakai na wake zao. Mienendo yao inatia aibu.
 
Mengine yote anaweza kufanikisha lakini kwa hili hapana!!licha ya hao maaskari nao ndio wateja wao ,
Hata lile la machinga haiwezi na ndio maana karukia kwa hao makahaba.

Ni vyema akijifunza kwa Samson aliyeingia kichwa kichwa kwa kahaba Delilah.

Makala wahurumia polisi usiwape hii kazi watatoboa siri mbele ya makahaba then watobolewe macho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…