RC Makalla, futa amri ya kuzuia watu kunywa bia mpaka muda wa kazi uishe, amri ambayo iliwekwa na Makonda

RC Makalla, futa amri ya kuzuia watu kunywa bia mpaka muda wa kazi uishe, amri ambayo iliwekwa na Makonda

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Dodoma wameweza kufuta amri ya kijinga ya kuzuia watu kunywa bia muda wa asubuhi kwa kisingizio cha kufanyakazi. Kazi ambayo pia haipo.

Sasa Amos Makala ebu futilia mbali amri ambayo iliwekwa na Makonda zama za utawala ambao haukuwa rafiki na Wafanyabiashara. Jeshi la polisi wanatumia marufuku hii kama sehemu ya kunyanyasa raia na kujipatia Rushwa.

Mama kasema anafungua nchi sasa sisi wengine kazi zetu hazipp serikalini inakuwaje mnatukera.
 
Sisi wengine ni walinzi wa shift za usiku. Mchana kwetu ndio usiku, asubuhi ndio jioni. Kwanini tusinywe wakati muda wetu wa kazi umeshaisha?
 
Mbona tunakunywa bia kuanzia asubuhi kama kawaida tu?
Dodoma wameweza kufuta amri ya kijinga ya kuzuia watu kunywa bia muda wa asubuhi kwa kisingizio cha kufanyakazi. Kazi ambayo pia haipo.

Sasa Amos Makala ebu futilia mbali amri ambayo iliwekwa na Makonda zama za utawala ambao haukuwa rafiki na Wafanyabiashara. Jeshi la polisi wanatumia marufuku hii kama sehemu ya kunyanyasa raia na kujipatia Rushwa.

Mama kasema anafungua nchi sasa sisi wengine kazi zetu hazipp serikalini inakuwaje mnatukera.
 
Tupo kwenye ulimwengu ambao huduma zinatakiwa zipatikane 24 hrs. Watu wakafanye kazi, hiyo serikali ya CCM imetoa ajira ngapi mpk sasa?
Mpumbafu yule alifuta ajira halafu akazuia bar watu wasinywe pombe wakafanye kazi. Hizo kazi gani?
Mtu awe huru, mtu akienda bar, anaenda kunywa kwa pesa yako?
 
Tukinywa supu michemsho asubuhi tunashushia bia.

Tukila mchana choma, rosti au ugali tunashushia bia

Tukila usiku pia tunashushia bia.

Kutwa mara 3
 
Hii sheria ingeangalia mazingira. Ila bahati nzuri maeneo ya kivuvi hawakuijari sana. Maana maeneo haya mchana ndo usiku. Watu wanaanza kutoka kazini saa 10 usiku mpaka saa5 asubuhi. Mchana ndo usiku wao na jioni wanaingia job
 
Wapi huko dsm wanakataza nije na kikosi kazi tuwafungulie kujiamini asubuhi kweupe.. li jack daniel kubwa kabisa na lisupu la kichwa
 
Kwani amri bado ipo?sahv watu wanagonga bia asubuhi mapema kabisa tena wazi bila kujificha sikujua hio amri bado ipo
 
Nadhani Mhe. Makonda hii amri alikuja kuitengua kipindi akiwa RC DSM
 
Mbona watu wanagonga bia mda wote hapa DSM
Weweee!!ina tegemea na maeneo, kuna baadhi ya maeneo askari wameshafanya biashara muda wote wa asubuhi ni kuzunguka kwenye mabaa kwa tafuta wanaokunywa pombe muda huo, hasa màeneo ya tabata, na wakiwakamata huwa ni kuchukua pesa tu na kuwaacha!!
 
Back
Top Bottom