RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Hii nchi inaenda kama gari bovu!

2025 ikikaribia, wataruhusiwa Kurudi katika maeneo hayo na pongezi zitatolewa.
2025 mbali mkuu, siku tatu watu watasahau jamaa watadunda kama kawaida siku zinaenda hakuna jipya, ukiondoa wamachinga malori saa hii ndio shida kuliko
Hapo kariakoo hapafai ni kama hakuna serikali,
Ila madhara yake makubwa sana
 
Taratibu za Uongozi nchini zinashangaza sana. Walikuwa wapi wakati haya yakianza, kwani hakuna wasimamizi wa hayo maeneo ambayo wangetakiwa kuwaondoa pindi tu wanapoanza hizo biashara? Haya matatizo yapo sehemu nyingi sana Dar. Kuna watu wamejenga katikati ya hifadhi za barabara na wamepewa hadi hati miliki za viwanja hivyo na "building permit".
 
Hiyo picha ya kwanza hapo juu, imenisababisha nianze kujadili mengine badala ya mada. Kuna kina baba tumefikia aina hiyo ya unene? Huyu bwana mwenye kishati kidooogo kama cha mwanae hapo ni machinga ama nae ni kutoka kwa kina Makala? Hivi vitambi vipo dar tu bilashaka
 
Pale mwenge ile barabara ya kuingia walishafanya yao, kuingia au kugeuza gari ni mtihani hawataki hata usogelee vibanda vyao.
Hao wote mijini waondolewe tu, na serikali ihakikishe hakuna mtu kurudi kuachia ili kuirudisha miji yetu iwe safi! Kila nchi ili iendelee vizuri , mipango miji na usafi utafanikiwa zaidi kwa kuwa na utaratibu wa kila mtu kufuata sheria zilizowekwa na sio kuongozwa na mihemko ya kisiasa.... matokeo yake ndo haya tunayaona vurugu mechi ktk miji yote! Kaaazi kwelikweli.
 
Big up Makala Songa mbele,
Tunapata shida sana watembea kwa miguu na hata kwa wenye magari.

Ila je,kiongozi wa machifu umecheck nae isije kuwa kama kiongozi flani wa moro.
 
unashauri nini kifanyike ?
 
Huyu sasa ndio atairudisha Dar kwenye hadhi yake
 
At last Serikali imeamka toka usingizi wa miaka mingi.
 
Sio rahisi kama anavyofikiria. Kutoa amri ni jambo moja lakini kuiweka kwenye vitendo sio rahisi. Watu hawa waliojikusanya na kuwekeza miaka'zaidi ya mitatu kwenye huo utaratibu utawaondoa kwa juma moja? Haiwezekani! Kuwaondoa hawa wa machinga kirahisi rahisi tu. It is a process which needs a big brain behind it.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…