RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

RC Makalla: Machinga wote Dar walio katika hifadhi ya barabara, Wataondolewa na vibanda vyao kuanzia Septemba 13, 2021

Bahati mbaya ni kwamba hayo maneno yake ni upepo tu yatapita...

Imeshazoeleka viongozi kuongea tu na maneno yao kupita...

Nani anayekumbuka Manzese ya zamani, Manzese iliyosafishwa na tazama Manzese ya sasa...
 
huyu mkuu wa mkoa anafanya cheap politics haya ni mambo minor sana, jiji hili lina changamoto kubwa na nyingi kuliko mambo ya wamachinga mfano miundo mbinu mibovu, wanafunzi kukaa chini, uchafu, hospitali hamna tiba ya uhakika
Kwa wanaomjua mh.RC Makalla watakushangaa....

Huyu ni kiongozi MWELEDI ,MWENYE MSIMAMO WA HEKIMA NA MNYOOSHA MAELEZO.....

Fuatilia ziara zake alizokuwa anaongea na WANANCHI juu ya changamoto zao.....

#SiempreJMT
 
Vibanda vivunjwe tu,hadhi ya mji irejee. Wamchinga warusiwe kufanya biashara kuanza saa kumi na moja jioni, vibanda marufuku.
 
Kwani dikteta wa kike anasemaje
FB_IMG_16307140795615105.jpg
 
Hakuna mwenye uwezo huo.

Hakuna mwenye kuweza kuwatoa wamachinga.

Makala hajawahi fanya jambo likakamilika.

Mkitaka mji uwe safi, Wamurudishe Makonda aje atunishe misuri yake. Wakishindwa huyo lambda Mtaka.

Kuwa ondoa machinga kunahitaji mtu atumie nguvu sana ama mipango mathubuti.

Machinga kama wa pale Mbezi huwezi ukawatoa hivihivi. Ni wengi mno afu hawana pa kwenda. Serikali ijipange. Ila Makala tu hawezi kwa kweli.
Mtatoka tu, imevunjwa misikiti,makanisa,taasisi za kiserikali inshindwe nyie...
Halafu mnajiona watu spesho Sana ,subirini..

I promise you utatoka (in manara's voice)
 
Wakitolewa huko na mikoa mingine itafuata nyayo.
 
Mtatoka tu, imevunjwa misikiti,makanisa,taasisi za kiserikali inshindwe nyie...
Halafu mnajiona watu spesho Sana ,subirini..

I promise you utatoka (in manara's voice)
Usidanganyike wewe.

Machinga ndio wapiga kura wa CCM na wako kimkakati.

Subiri tamko kutoka juu kwamba Machinga wasibughuziwe!
 
Kwa hali ilivo kwa maeneo kama Mbezi mwisho ni hatari sana. Wamekaba njia zote za waenda kwa miguu na Sasa hata magari kupita ni shida. Wasiwasi wangu ni he watawatoaje na pia watawapeleka wapi?
 
Kivuruge aliyejipa jina la mtetezi wa wanyonge ndio kaleta balaa lote hilo kwa kutafuta sifa za kijinga, haiwezekani useme machinga wafanye biashara kokote kama mji wote wanaishi wao tu.
Hujiulizi kama kuna wengine pia wana haki ya kutumia maeneo hayo hayo kwa shughuli zao nyingine?
 
Usidanganyike wewe.

Machinga ndio wapiga kura wa CCM na wako kimkakati.

Subiri tamko kutoka juu kwamba Machinga wasibughuziwe!
Na wewe machinga ni kero. Sasa kama hapo hoja kuu ni watembea kwa miguu kukosa nafasi ya kupita. Kawachunguze hao machinga wako kama wana vitambulisho vya kupiga kura
 
Wamachinga wako njiani kwa sababu kuna wateja. Nadhani kila mtu anajua tatizo sio wauzaji(machinga), ni utamaduni wa wanunuzi(wateja) kupenda kununua vitu kiholela holela. Kuna maeneno kariakoo sioni yana tofauti gani na gulio la kinondoni biafra au kunduchi mtongani.

Sent from my SM-G930L using JamiiForums mobile app
 
Afadhali kama Mbezi ni tatizo kubwa kuanzia pale kwa Msuguli. Watu wanaingia mpaka ndani ya njia nane kufanya biashara hata hawaogopi kupelekwa akhera bila mpangilio. Mbezi mwisho ni shida machinga walianza kuzibamaeneo ya wenda kwa miguu, wakahamia kwenye mifereji ya maji na sasa wamehamia kabisa barabarani kiasi kwamba kupita ni shida kubwa. Wakati fulani niliuliza nani anahusika na usalama wa watu hawa kati ya Tanroads na manispaa. Maana hii njia ya Mbezi iliyozibwa kwa sehemu kubwa na machinga ndiyo anayopita mkurugenzi wa manispaa kwenda na kurudi kwake Malambamawili ikajiuliza ina maana haoni hii karaha au kwakuwa yeye anakula kiyoyozi cha mil 400?
 
Na wewe machinga ni kero. Sasa kama hapo hoja kuu ni watembea kwa miguu kukosa nafasi ya kupita. Kawachunguze hao machinga wako kama wana vitambulisho vya kupiga kura
Kitambulisho cha mpiga kura ni muhimu kwa Chadema siyo CCM!
 
Machinga wa Mizani ya Mikese wanaouza miwa ya paketi na korosho nao ni kero kubwa. Makala njoo na huku umsaidie RC mwenzako
 
Back
Top Bottom