RC Makalla: Mkoa wa Dar upo salama Baada ya kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 135 na Vifaa mbalimbali vilivyoibwa

RC Makalla: Mkoa wa Dar upo salama Baada ya kufanikiwa kuwakamata Watuhumiwa 135 na Vifaa mbalimbali vilivyoibwa

Kwanini tuendeshe operation ya nguvu wakati wa matukio wakati tuna Askari wa kutosha.
 
Lakini kuna swali la kuuliza hapa.

Polisi hawafanyi kazi hadi iwepo 'operation' ya jambo maalum?
Polisi walikuwa hawajui kuwa 'Panya Road' wanasumbua wananchi kabla ya hii operation?

Anazungumzia vituo vya polisi kufanya kazi masaa 24; kabla ya hapo vilikuwa havifanyi kazi baadhi ya masaa?
Kwa hiyo baada ya saa 12 jioni basi na polisi wanaenda kulala, sasa kuna faida gani ya kuwa na polisi kwenye nchi hii. Hapo mnawaambia majambazi sasa ni wakati wenu muanze kuwaumiza watu. Polisi kwenye nchi za wenzetu wanafanya kazi masaa 24, wetu wanafanya zamu ya masaa 12, ikifika jioni ndiyo muda wao wa kazi umeisha, kwa jinsi hiyo hii nchi vibaka na majambazi hawataisha. Hizi operation za kupewa taarifa za uongo haziaminiki, si ajabu hata waliouawa si hao panya road, ni kundi la vijana wanaenda zao kwenye mambo yao wakakutwa barabarani ikawa bahati mbaya, wameuawa kuficha ushahidi, zipo wapi picha na video za polisi wakipambana na hao Panya road? Au wananchi walishuhudia hayo mapambano wapi? Msitudanganye, wewe mkuu wa mkoa ndiyo bure kabisa.
 
Back
Top Bottom