Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
Kwanza kabisa kuondolewa kwa mifuko ya plastiki bado hakujafanya mazingira kuwa safi. Nini tatizo kwa mkoa wa Dar es Salaam?
Jibu ni rahisi tu, tatizo ni msongamano wa watu pamoja na wafanyabishara wadogo (machinga) huu ndio ukweli. Japo ili kufanya mkoa huu kuwa safi si lazma uwatoe ila unaweza kutengeneza mtandao wa usafi na mkoa ukang'aa.
Cha kwanza utaratibu wa usafi unapaswa kuwa ni ule ule ila wawepo wasimamizi (walinzi) wa kila siku. Kwa sababu ya ugumu wa kumfuatilia mtu alietupa taka sehemu fulani mashauri haya.
Upitishwe sheria ndogo kwa ,mfanya biashara yeyote, wakaazi wa mitaani na wapangaji wana wajibu wa kusimamia usafi kwenye maeneo yao,mkaguzi wa takataka akija na kukuta kuna uchafu/takataka katika eneo alilopo atapigwa faini ya 50,000/= bila kujali katupa yeye au mwingine.
Kama utamwona mtupaji wa taka si lazma umkamate,unaweza kuzungumza nae na kumpa elimu kuhusu usafi,huku ikisisitiza achukue taka yake aondoke nayo kama akikataa uombe usaidizi kwa raia wengine mumkamate.
Vituo vya kuwafikisha wachafuzi viwe serikali za mtaa kwanza sababu ndio zipo nyingi kuliko ofisi nyingine. Akilipa 50,000 kamishileni ya mkamataji iwe 20,000(ili kuhamasisha)
Uwepo wa sheria hiyo utafanya kila mtu awe makini kwenye eneo atakalokuwepo iwe kasimama stendi,mchoma mahindi, mmachinga hata majumbani pia.
UMAKINI UTAKUWA HIVI KWA KILA MTU
Kila mtu akuwa analinda eneo alilokuepo na hata kama kakuta uchafu ataokota na kuweka sehemu husika hata kama hajatupa yeye sababu tayari sheria hiyo inambana.
Mfano: nimeenda kituo cha daladala nasubiri gari lakini naona kuna chupa zimetupwa hovyo huku pembeni kuna dastibin itanilazimu kuokota na kuzihifadhi sababu tayari naogopa bwana afya au usafi akinikuta nimesimama hapo na hizo chupa zipo atanipiga faini mimi japo sijatupa.
Ili kutofautisha wasimamizi na matapeli, wasimamizi wapewe vitambulisho maalumu vitakavyomtambulisha au kumtofautisha na raia wa kawaida.
Tukifuata huu utaratibu ni nani atakubali kuoigwa faini? Nani atakubali kukaa au kusimama na uchafu? Nani atakwepa kufanya usafi tena?

Upvote
3