Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, leo Desemba 13, 2022 ameendelea na ziara ya ukaguzi Maendeleo ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa Mkoa huo ambapo ilikuwa zamu ya Wilaya ya Temeke, ameelekeza Halmashauri hiyo kuhakikisha madarasa yanakamilika kabla ya Desemba 30, 2022.
RC Makalla amempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi sahihi ya kutoa fedha ili kuhakikisha kila Mwanafunzi anasoma kwenye mazingira Bora na kuwaondolea Wazazi usumbufu wa michango Kama miaka ya nyuma.
Aidha, RC Makalla ameshuhudia Ujenzi wa Madarasa ukiendelea vizuri ambapo Wilaya ya Temeke ilipokea Shilingi Bilioni 4.1 kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa 207 ikiwemo ya Gorofa na Mtawanyiko ambapo mpaka Sasa Madarasa 97 yapo kwenye ngazi ya Ujenzi wa Msingi, 32 ukuta, 67 Yanaezekwa na 11 Ujenzi unaanza kesho Baada ya kupatikana kwa maeneo.
RC Makalla pia amepokea taarifa ya Wilaya juu ya idadi ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na masomo mwezi January mwakani ambapo Kwa Shule za Awali wanaotarajiwa ni wanafunzi 6,343, Msingi wanafunzi 26,000 na Sekondari 23,000.
Ifahamike kuwa Mkoa wa Dar es Salaam ulipokea zaidi ya Shilingi Bilioni 12.3 kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa kwaajili ya wanafunzi wa Shule za Awali, Msingi na Sekondari ambapo pia amesisitiza Ubora wa Majengo yatakayojengwa.