RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

kwa haya yanayo endelea mkuu angempumzisha tu uyu kijana ata kma ana singiziwa kuondoa hili wingu jeusi
 
Habari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.

Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!

Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.
Ila story imetengenezwa vizuri,kwa siye wengi wa vijijini tusioijua Dar vizuri wala hizo ofisi za clouds zinafanana vipi hatukawii kuamini.
 
MAKONDA AVAMIA CLOUDS KWA MITUTU YA BUNDUKI : [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] CHUPUCHUPU KUUWAWA.

Jengo la Clouds Media Group lililopo Mikocheni B jana lilishuhudia sekeseke la aina yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia akiwa na Walinzi wenye Bunduki.

Tukio hilo tukoea majira ya Usiku wakati kipindi SHILAWADU kikiwa hewani ambapo Makonda alivamia kwa lengo la kushinikiza Shilawadu waonyeshe mahojiano yenye lengo la kumchafua Askofu Gwajima.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba, mwanzoni wiki 2 zilizopita, SHILAWADU walipigiwa simu na watu wasiojulikana wakieleza kwamba wana 'ubuyu' mzito wa kuhusu Askofu Gwajima na mwanamke anayedaiwa kuzaa nae. Mwanzo Shilawadu walikataa habari hiyo, lakini siku moja walikutana na Makonda akawashawishi SHILAWADU wafuatilie stori hiyo. Kama kawaida yao kupenda umbea, SHILAWADU wakiongozwa na Soudy Brown walimtafuta mwanamke anayedaiwa kuzaa na Gwajima kisha wakamhoji.

Hata hivyo, kwa kuhofia nguvu ya Gwajima katika kupambana na shutuma dhidi yake, na kwa kuzingatia maadili ya kazi, SHILAWADU waligoma kurusha habari hiyo hewani mpaka wapate kauli za upande wa pili ( upande wa Gwajima ). Baada ya kuhangaika huku na kule , SHILAWADU walishindwa kupata upande wa pili wa habari ( walishindwa kubalance story ).

Kutokana na hilo, na kujua kwamba Gwajima asingewaacha salama kwa kutoa story ya uongo dhidi yake, [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] na wasimamizi wa vipindi wa Clouds Tv waliamua kuachana kabisa na story hiyo.

MAKONDA ANAINGIAJE? : Imefahamika kwamba watu ambao walipiga simu kwa Shilawadu kuhusu uwepo wa Mwanamke huyo ni watu wa Makonda. Makonda alitaka story hiyo itolewe kupitia [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] ambao wana kawaida ya kuripoti matukio ya Watoto/wanawake waliokataliwa. Kwa kuwa Makonda ana marafiki wengi pale Clouds, aliamini kwamba story hiyo lazima ingetolewa na hivyo kumchafua adui yake GWAJIMA ( kuzima sakata la vyeti ).

Akiwa nyumbani kwake Masaki, Makonda alikaa kwenye Tv yake Ijumaa kusubiri SHILAWADU wamvue nguo Gwajima. Cha kumsikitisha, Makonda alipata habari kwamba SHILAWADU wamegoma kupeleka habari hiyo. Hata viongozi akiwemo swahiba wake Ruge walikaataa kabisa kupeleka habari ambayo haiko 'balanced' na mbaya zaidi inawaingiza kwenye vita na mtu wa aina ya Gwajima.

Kama kawaida yake, Makonda aliamua kutumia ubabe. Kwa kuwa amezoea kuingia Clouds, Makonda alifahamu kuwa muda huo viongozi hawapo na watu waliopo anawamudu. Hivyo aliamua kwenda Clouds kuhakikisha Shilawadu wanaonyesha habari hiyo ya kumchafua Gwajima. Hivyo alibeba wanaume zaidi ya 8 wakiwa wamebeba silaha za moto.

Alipofika Clouds, walinzi wa Getini walimruhusu kupita yeye na gari iliyokuwa nyumba yake akisema ni rafiki zake wamekuja mara mara moja kwenye SOSOO FRESH kwani Adamu Mchomvu amewaalika. Lakini alipofika Reception, Mlinzi wa zamu alisitia baada ya kuona Makonda amekuja na watu wengi. NA HAPO NDIPO KASHESHE ILIANZA.

Walinzi wa Makonda walitoa Bunduki, walimtishia Mlinzi wakampiga sana na wakatumia nguvu kubwa hadi walifanikiwa kuingia ndani. Walipofika na Bunduki zao, Makonda aliamuru kila mtu kukaa alipo huku akilazimisha habari ya Gwajima iende. Kwisa kama kiongozi wa kipindi ndiye ambaye alipingwa mitama na ngumi za kutosha.

Kwa walioangalia kipindi wanajua kwamba kipindi hakikuisha, hiyo ni kutokana na kwamba Makonda na waligawa kipigo cha maana kwa Shilawadu kisha wakawabeba kwenda nao nje akisema wanaenda Cental.

Pia alitumia Bunduki kuwalazimisha Shilawadu wampe Video ya Mama anayedaiwa kuzaaa na Gwajima ( alipewa ). Makonda aliwaambia wapambe wake kama Shilawadu wamekataa kuonyesha habari hiyo baasi yeye atahakikisha inasambaa kupitia mitandao ya kijamii.

Hivi sasa Shilawadu hawako sawa kisaikolojia huku Suod Brown akiwa hana amani kwani alipigwa picha na Makonda alimuambia kama anaogopa kumdhalilisha Gwajima baasi yeye atadhalilishwa kwani Sura yake itawekwa hadharani kila mtu afahamu.

Baadae Makonda aliondoka baada ya kupigiwa simu ambayo haijulikani nani alipiga lakini Makonda alipoondoka Ruge alingia Clouds akiwa na watu huku na yeye amebeba bastola. Inaaminika ile simu ilipigwa kumuambia aondoke maana Ruge anakuja.

Source : Hidden.
 
tafadhari mkuu mwenye kaya jpm.unamsikia huyu kijana wako anavyofanya au unaziba masikio kwa makusudi.maana anautumia ulinzi vibaya sasa.huyu kijana hatakama anafanya vizuri kwa hapo alipofikia atakudhalilisha hata wewe.
 
Na Raisi ndo support wa ujinga wa Bashite ndo maana walikuwa wanajifanya wana uchungu kumbe wanaonea wengine. Mungu huwafichua wanafiki.
Yaani hapa kila siku naombea JPM asimtumbue Bashite leo wala kesho!! Aendelee kumlea lea hivyo hivyo angalau kwa wiki zingine 2 au 3 ili waendelee kuogeshana vinyesi!!!! Manake hili la Bashite ndo linatoa picha halisi ya JPM....
 
Umeona enh?! Mi watu nimewaambia jana Mkulu alikuwa standby akisubiri kula ubuyu wa Gwajima live bila chenga halafu jamaa wamemzingua!!!
Nawashauri waandika makala wakitegemea zimfikie basi waanze kuziandika katika magazeti ya udaku.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Baba mwenye nyumba hasipo kuwa mwepesi wa kuchutama raia wataendelea kushangilia "zakaria" zilivyo wazi.
 
Mkuu hapana unyang'anyi sio lazima hadi risasi itumike na kuhusu unyang'anyi wa kutumia nguvu tena majira ya usiku huku kukiwa na smg na watu kupigwa na huenda ikawa wamejeruhiwa wewe unasema armed robbery haipo ? pitia tena mazingira ya tukio then uje uandike hiyo ni pure Armed robbery.
 
Back
Top Bottom