RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

Jamani clip ishasambaaa walivovamiwa ...
Nchi yetu tunakwenda wapi huyu ndo lumumba mlikua mnam defend na baadhi ya watu humu ....
Hivi imefikia mahali kwamba mtu anaweza kuingia kazini kwangu na kunitishia kwa silaha ya kivita ni kuniamuru nifanye against na taratibu na sheria za kazi yangu ....oneni sasa ....video live kabisa mtajificha wapi
Rais wake anaemtetea atamficha wapi katika hili ....
 
Mkuu footage imekuvua nguo live.
 
Si umeona CCTV iliyorushwa na Gwajima ikionesha askari wakiingia Clouds wakiwa na Makonda?! Makonda anaenda Clouds TV saa tano kasorobo usiku kufanya nini!!!!

Zile habari ambazo kuna wapuuzi wachache jana walikuwa wanajifanya kukanusha sasa kuna kila dalili kwamba ni kweli!!!
 
Ni utoto tu akikua ataacha,tunataka kujua hao walinzi ni security group au ni hawa wa mwigulu tunaowalipa sisi mshahara!
 
Ivi video ya kuingia iwekwe, afu video ya kupigwa mitama ambayo ndo ime-hold water ya ishu nzima isiwekwe!
Kuna ulazima gani wa kwenda shule sasa!
 
Tena hatari kabisa kumkabidhi jeshi mtu asiyeaminika,mualifu wa kugushi vyeti na identity ya mtu mwingine anaweza kutumia hilo jeshi kinyume na kuhatarisha amani ya nchi. Hili ni angalizo na ni aibu kwa nchi ya kistaarabu kama Tanzania kuona matukio ya aina hii. Ni kama Tanzania kwa sasa tunaongozwa na magenge ya kihalifu.

Ninapata wasiwasi ata ofisi za JF zinaweza kuvamiwa kwa style ya clouds kuvamiwa na kuhatarisha usalama wa watumiaji. Sidhani hili kama lipo sawa. Kuna ukakasi na kinyaa ndani ya sakata la bashite.

Ata akina Iddi Amini walianzia hivi hivi wakafanikiwa kufanya mapinduzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…