RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

~~~>>>Jana kwa mara ya kwanza nilipoona huo Ujumbe ukisambaa...

~~~>>>Sikuuamini kwakuwa nilijua kwa akili za RC hawezi kufanya tukio la kijinga namna ile

~~~>>>Leo nikaona habari Facebook ya Janes Mwenda.. Nikajua enhee inawezekana kweli.

Mara JF nauona tena huu uzi na Video...... Naona kuna umuhimu wa kumpima huyu jamaa akili.
 
Hiyo radio naichukia sna
 
Mashehe wanapewa pesa wanamuombea mtu muhuni sasa amewaumbua inawezekana yale maombi aliwalazimisha mumuombee
 
Kwa usalama wa hospitali, hapo kwenye jina na namba pamezibwa angalia vizuri, hatuna haja ya kuwachosha maana mkitaka mnaweza kwenda kupima dNA, hivi vitu rahisi sana, kadi isikuchoshe.
kama ni kweli yann kuficha?
 
Mimi nasubiri siku ambayo Sizonje atakapokuwa anamwapisha RC mpya wa Dar sijui atampa Usia gani i.e kufanya yote mazuri yale ya mtangulizi wake.
 
Hiyo video ni ya Bongo Movie???
 
Haya mambo (kwa maoni yangu) yanachukua muonekano wa ukabila. Magufuli, Makonda na mkurugenzi mkuu wa Clouds wote ni wasukuma. Nikizidi kuhisi ni kwamba hata cdf naye ni wa huko huko pamoja na mwanasheria wa serikali.
Hivyo basi, kwa kitendo cha bw. Bashite kumtukana yule mama (mwenye elimu nzuri kumzidi) pamoja na kuthubutu kusema ukimwona yeye umemwona Mungu wa Dar bila kukemewa na mamlaka yaliyomuweka hapo alipo ni dhahiri kuna anachojiaminishia.
Ila sasa, kitendo cha kuvamia kituo cha habari na kulazimisha watangazaji warushe kile ambacho Makonda alitaka kiliwatisha wengi na kitakuwa kimwewaudhi wamiliki wa clouds. Hiki kitendo hakina tofauti na UHAINI, yaani pale angeweza kuchukua mike na kuamuru kamera upande wake na kutangaza AMEPINDUA SERIKALI! Kizaa zaa gani kingetokea?
Najua mkurungenzi mdogo Ruge hatokubali, lazima jambo litendeke kuhusu tukio hili.
 
Sipati Picha bashite akifutwa kazi atakuwaje na mkoa utakuwaje
Kwa sasa ilitakiwa JPM awajibike kwa kosa la kufumbia macho tuhuma za wazi, tena hata kuitisha uchunguzi ameshindwa juu ya vyeti feki. Yeye alichokifanya ni kiwatisha wabunge wa ccm ili wasimwajibishe makonda na pm. Kwa maana nyingine analinda uhalifu
 
Mpaka leo bado Makonda yupo kwenye ukuu wa mkoa? Rais wangu Magufuli please tenda tafadhali roho zetu zipoe huyu asikushushie imani yetu kwako kwani tunakuamini sana Kiongozi wetu muweke tu pembeni sheria ichukue mkondo wake nchi isonge mbele bado tuna mambo mengi sana ya kufanya Mungu akufanyie wepesi
 
Tunapuuzaje wakati wahusika hawajatoa tamko, video tunaiona mitandaoni na si official kwenye kipindi... Kipindi kimerushwa hakijaisha, video ya makonda na polisi tumeiona... Upo vizuri upstairs?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…