RC Makonda avamia Clouds na kuwatisha SHILAWADU

Hiyo video imewekwa kwenye account ya hao vijana au imewekwa kwenye account za watu gani huko Instagram
 
Tupia basi hizo clips aisee....
 
MAKONDA AVAMIA CLOUDS KWA MITUTU YA BUNDUKI : [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] CHUPUCHUPU KUUAWA.

Jengo la Clouds Media Group lililopo Mikocheni B jana lilishuhudia sekeseke la aina yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia akiwa na Walinzi wenye Bunduki.

Tukio hilo tukoea majira ya Usiku wakati kipindi SHILAWADU kikiwa hewani ambapo Makonda alivamia kwa lengo la kushinikiza Shilawadu waonyeshe mahojiano yenye lengo la kumchafua Askofu Gwajima.

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba, mwanzoni wiki 2 zilizopita, SHILAWADU walipigiwa simu na watu wasiojulikana wakieleza kwamba wana 'ubuyu' mzito wa kuhusu Askofu Gwajima na mwanamke anayedaiwa kuzaa nae. Mwanzo Shilawadu walikataa habari hiyo, lakini siku moja walikutana na Makonda akawashawishi SHILAWADU wafuatilie stori hiyo. Kama kawaida yao kupenda umbea, SHILAWADU wakiongozwa na Soudy Brown walimtafuta mwanamke anayedaiwa kuzaa na Gwajima kisha wakamhoji.

Hata hivyo, kwa kuhofia nguvu ya Gwajima katika kupambana na shutuma dhidi yake, na kwa kuzingatia maadili ya kazi, SHILAWADU waligoma kurusha habari hiyo hewani mpaka wapate kauli za upande wa pili ( upande wa Gwajima ). Baada ya kuhangaika huku na kule , SHILAWADU walishindwa kupata upande wa pili wa habari ( walishindwa kubalance story ).

Kutokana na hilo, na kujua kwamba Gwajima asingewaacha salama kwa kutoa story ya uongo dhidi yake, [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] na wasimamizi wa vipindi wa Clouds Tv waliamua kuachana kabisa na story hiyo.

MAKONDA ANAINGIAJE? : Imefahamika kwamba watu ambao walipiga simu kwa Shilawadu kuhusu uwepo wa Mwanamke huyo ni watu wa Makonda. Makonda alitaka story hiyo itolewe kupitia [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] ambao wana kawaida ya kuripoti matukio ya Watoto/wanawake waliokataliwa. Kwa kuwa Makonda ana marafiki wengi pale Clouds, aliamini kwamba story hiyo lazima ingetolewa na hivyo kumchafua adui yake GWAJIMA ( kuzima sakata la vyeti ).

Akiwa nyumbani kwake Masaki, Makonda alikaa kwenye Tv yake Ijumaa kusubiri SHILAWADU wamvue nguo Gwajima. Cha kumsikitisha, Makonda alipata habari kwamba SHILAWADU wamegoma kupeleka habari hiyo. Hata viongozi akiwemo swahiba wake Ruge walikaataa kabisa kupeleka habari ambayo haiko 'balanced' na mbaya zaidi inawaingiza kwenye vita na mtu wa aina ya Gwajima.

Kama kawaida yake, Makonda aliamua kutumia ubabe. Kwa kuwa amezoea kuingia Clouds, Makonda alifahamu kuwa muda huo viongozi hawapo na watu waliopo anawamudu. Hivyo aliamua kwenda Clouds kuhakikisha Shilawadu wanaonyesha habari hiyo ya kumchafua Gwajima. Hivyo alibeba wanaume zaidi ya 8 wakiwa wamebeba silaha za moto.

Alipofika Clouds, walinzi wa Getini walimruhusu kupita yeye na gari iliyokuwa nyumba yake akisema ni rafiki zake wamekuja mara mara moja kwenye SOSOO FRESH kwani Adamu Mchomvu amewaalika. Lakini alipofika Reception, Mlinzi wa zamu alisitia baada ya kuona Makonda amekuja na watu wengi. NA HAPO NDIPO KASHESHE ILIANZA.

Walinzi wa Makonda walitoa Bunduki, walimtishia Mlinzi wakampiga sana na wakatumia nguvu kubwa hadi walifanikiwa kuingia ndani. Walipofika na Bunduki zao, Makonda aliamuru kila mtu kukaa alipo huku akilazimisha habari ya Gwajima iende. Kwisa kama kiongozi wa kipindi ndiye ambaye alipingwa mitama na ngumi za kutosha.

Kwa walioangalia kipindi wanajua kwamba kipindi hakikuisha, hiyo ni kutokana na kwamba Makonda na waligawa kipigo cha maana kwa Shilawadu kisha wakawabeba kwenda nao nje akisema wanaenda Cental.

Pia alitumia Bunduki kuwalazimisha Shilawadu wampe Video ya Mama anayedaiwa kuzaaa na Gwajima ( alipewa ). Makonda aliwaambia wapambe wake kama Shilawadu wamekataa kuonyesha habari hiyo baasi yeye atahakikisha inasambaa kupitia mitandao ya kijamii.

Hivi sasa Shilawadu hawako sawa kisaikolojia huku Suod Brown akiwa hana amani kwani alipigwa picha na Makonda alimuambia kama anaogopa kumdhalilisha Gwajima baasi yeye atadhalilishwa kwani Sura yake itawekwa hadharani kila mtu afahamu.

Baadae Makonda aliondoka baada ya kupigiwa simu ambayo haijulikani nani alipiga lakini Makonda alipoondoka Ruge alingia Clouds akiwa na watu huku na yeye amebeba bastola. Inaaminika ile simu ilipigwa kumuambia aondoke maana Ruge anakuja.

Source : Hidden.
 
Wewe ni ruge?
 
Acha awachape tu makofi hao.
Mtoto umleavyo....
 
Hii story wenyewe mbona imrkaa ko shilawadu shilawadu kuanzia neno la kwanza mpaka la mwisho.

I will be the last one to agree with this story .
Asante mkuu Kwa kurejesha avatar picha yako inayoendana na meinkempf. Naona umerudi jamvin Kwa kas ya ajab baada ya kupotea Kwa muda. Nakumbuka enzi za magu akiwa bado mgen ikulu ulikuwa unashusha nondo humu jamvin ukimsifu. Nakumbuka nikiwa mgen JF 2013 ulikuwa unapenda kutumia neno "vitu vyenye ncha kali" Yani visu nk na "vitu vyenye ncha kali vinavyoruka hewan Kwa kas ya ajab" risas. Nakumbuka nondo zako za yule housegeli uganda aliyemtesa mtoto
 
Mi naamini kwa kiasi fulani!!! Clips kuhusu huyo mwanamke zinasambazwa na Le Mutuz na anaonekana alikuwa anahojiwa na Soudy Brown!!!

Kwavile hicho kipindi huwa siangaliaji; mwanzoni nilidhani kilirushwa jana Clouds!! Sasa kama hazijarushwa na Clouds, basi kuna uwezekano ni kweli kwa sababu ni kweli hizo clips zipo!!!
 
Acha uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…