minyoo
JF-Expert Member
- May 25, 2013
- 22,405
- 21,100
Kama Waziri wa Elimu kajificha hathubutu kutoa Tamko unadhani Tume ya maadili watathubu kusema chochote?Hivi tume ya maadili ya viongozi ipo kweli na inafanya kazi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama Waziri wa Elimu kajificha hathubutu kutoa Tamko unadhani Tume ya maadili watathubu kusema chochote?Hivi tume ya maadili ya viongozi ipo kweli na inafanya kazi?
Tupia basi hizo clips aisee....=====
Msomaji, vema pia ukasoma hapa > Mwanamama kupitia Uhuru FM, adai kuzalishwa na Askofu Gwajima na kutelekezwa!
=====
Makonda hua anafika office za clouds mara kwa mara. Siku zingine anashinda hapo mpaka jioni. Siku ya Alhamis Makonda alifika office za Clouds Cha ajabu siku hiyo alikaa mpaka usiku akawa anamtafuta soudy Brown na Qwisser wa SHILAWADU muda huo walikuwa bado hawajafika kazini basi akawa anazungukazunguka tu ofisi hii anatokea ile kama mfanyakazi wa Clouds.
Kwenye Mida ya Saa kumi hivi akakutana na kina Soudy pamoja na prodyuza wa kipindi wakawa wanaongea kwa uficho hivi na usiri tukajua tu ni mambo ya kawaida ya kuhitaji uprivate lakini siku ile ulikuwa unatia mashaka sana.
Kumbe Makonda alikuja na Story ya mwanamke mmoja ambaye yeye Makonda alisema huyo mwanamke amezaa na mchungaji Gwajima na ametelekeza akawa anataka arekodiwe na ubuyu uruke kwenye kipindi cha SHILAWADU.
Basi wakakubalia kwa kuwa ni habari itabidi huyo mwanamke arekodiwe na kipindi kiruke siku ya jana lakini kawaida ya Kipindi cha SHILAWADU ubuyu ukipatikana lazima kila mtu apewe Natural Justice ya kusikilizwa pande zote mbili sababu huwa ndiyo kawaida ya kipindi.
Makonda siku hiyo hiyo ya Alhamisi akamwambia Soudy ajiandae then huyo mwanamke mnayemuona kwenye video na mtoto aliletwa na wasaidizi wa Makonda ahojiwe na Soudy Brown tayari kwa kurushwa kwa kipindi.
Siku ya Ijumaa ambayo ilikuwa ni jana SHILAWADU wakamtafuta Gwajima kwa upande wake kama anaifahamu hiyo ishu na je mwanamke huyo aliyetajwa ni kweli kwasababu tunaelewa ugomvi uliopo kati ya Makonda na Gwajima isijekuwa SHILAWADU wanatumika kuwafitinisha watu vibaya!
kwa bahati mbaya Gwajima hakupatikana jana ijumaa kwa ajili ya kurekodiwa na kufanyiwa mahojiano.
SHILAWADU wakatumia busara mpaka apatikane Gwajima scene ya Dada mwenye mtoto ziende kwa pamoja na ya mchungaji Gwajima kama kawaida ya POVU inavyokuwaga.
Jana usiku sasa kumbe Makonda alikuwa anafuatilia kipindi cha SHILAWADU aone kama kile kipande kitaruka hewani wapi ndiyo akaamua kuja Clouds na magari mawili yeye mwenyewe Makonda na Watu kama nane hivi wakiwa na Bunduki aina ya SMG geti la kawaida mlinzi alifungua geti kwasababu amezoeleka Mh anakujaga mjengoni wakafunguliwa kisha wakaingia ndani.
Walipofika reception wakazuiwa kuingia ndani sababu hatuna utaratibu wa kuruhusu wageni baada ya saa Nne usiku kuingia ndani ya Ofisi kama siyo mfanyakazi wa CLOUDS.
Alipoona wanazuiwa wakatoa bunduki zao mlinzi akashurutishwa afungue mlango kwa nguvu sababu walimtishia na Silaha mlimzi akafungua mlango wakaenda naye hadi studio kipindi kilikuwa kinaendelea hewani.
Makonda akawatoa nje Soudy na Mwenzake Qwisser akawauliza kwanini video aliyowaletea haijachezwa wakaelezea utaratibu jinsi utaratibu ulivyokuwa Qwisser wakati anajielezea akapigwa mtama akaanguka chini wakavamia mitambo ya transmission kwenye traycaster wakitaka kile kipande kirushwe hewani prodyuza wa kipindi akamuambia Makonda kwanini anavunja utaratibu na kutumia nguvu na ameshapewa utaratibu akapigwa na kitako cha Bunduki mgongoni akaanguka chini bahati mbaya kipindi kilikuwa kimefika mwisho.
Wakamshurutisha Prodyuza wa SHILAWADU anaitwa Chriss awape kile kipande wakaondoka naye wakati wanaondoka Ruge alikuja na Polisi akaingia lakini tayari walikuwa wameondoka ofisini wamechukua hicho kipande cha Video ya huyo mwanamke.
Hizo video zilichukuliwa kwa nguvu na Makonda na hao watu waliokuwa na Silaha inasemekana Makonda ana timu yake wanazisambaza kwa kasi na hatujui lengo lake ni nini.
Hata mkihitaji footage za Camera zipo jinsi tukio lilivyokuwa usiku wa jana.
====
Kutoka kwa wadau wa Clouds Media
Huyu Mzee zamani nilikuwa namtetea sana lakini anavyohangaika na Bashite hadi anatia huruma!!!Le-Mutuz kwa sasa limejikita kwa Makonda saa 24 linazunguka zunguka kwake kuokota chochote ni jitu lisilojitambua kwa kiasi kikubwa sana.
Wewe ni ruge?Habari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.
Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!
Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.
Asante mkuu Kwa kurejesha avatar picha yako inayoendana na meinkempf. Naona umerudi jamvin Kwa kas ya ajab baada ya kupotea Kwa muda. Nakumbuka enzi za magu akiwa bado mgen ikulu ulikuwa unashusha nondo humu jamvin ukimsifu. Nakumbuka nikiwa mgen JF 2013 ulikuwa unapenda kutumia neno "vitu vyenye ncha kali" Yani visu nk na "vitu vyenye ncha kali vinavyoruka hewan Kwa kas ya ajab" risas. Nakumbuka nondo zako za yule housegeli uganda aliyemtesa mtoto
Nakutaftaahahaaa rusha tukio lilivokuwa la sivo hatutokuamini
Mi naamini kwa kiasi fulani!!! Clips kuhusu huyo mwanamke zinasambazwa na Le Mutuz na anaonekana alikuwa anahojiwa na Soudy Brown!!!Napata ugumu kuamini hii habari bila ushahidi, ila pia kwa namna team Makonda wanavyopigana hii vita, nalazimika kuziamini tuhuma zote juu yao. Namna pekee kwa Mkulu, Makonda, na timu yao, ya kuwa-discredit Gwajima na Mange, ni kwa kumaliza utata dhidi ya authenticity ya elimu na identity ya Makonda. With that, hata tuhuma za kupiga dili chafu zitakosa nguvu.
Acha uongoHabari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.
Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!
Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.
Ndio anatafta namna ya kujiondoa on troublekama kuna video footage basi Bashite yupo in trouble!
[emoji23] [emoji23] umeongeza siku zangu za kuishi[emoji106]View attachment 483065 ukifariki kipindi hiki utamiss mengi Sana
Nenda akaunti ya Le Mutuz utaikuta!!!Hiyo video imewekwa kwenye account ya hao vijana au imewekwa kwenye account za watu gani huko Instagram