LUCIFER
Senior Member
- Aug 14, 2012
- 183
- 88
Hujaelewa nini mama,? Kwan huijui firigisi?Duuu.. Sijakuelewa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hujaelewa nini mama,? Kwan huijui firigisi?Duuu.. Sijakuelewa
Footage zimevuja mitandaoni na zinaonesha kila kitu we unaejidai ulikuepo mjengoni mda huo tukueleweje? Usikurupuke kuandika ili watu wajue kuwa nawe huwa unakuepo pale...Habari kama hizi za kichochezi na za uzushi ndizo zinazotuponza wanaJf mbona tuliokuepo mjengoni mda huo hatujasikia lolote na hakuna chochote kilichotokea.
Au umetumwa?
Clouds ni taasisi kubwa inayoongozwa kwa misingi na taratibu zake haiwezekani mtu from no where aje tu aingie mpaka peoduction bila kufata utaratibu!
Acha uzushi watanzania puuzeni hizi taarifa si za kweli!!.
Tehe tehe tehe yule anayejifanyaga Makonda oyeeeeeeeNa mimi sijamuona kabisa.
Ni kama kajitoa na jf
Faiza unalizungumziaje hili la bashite kuvamia studio za clouds?..kwa mujibu wa "video clip"..iliyopo humu jamvini.Paukwa
Pakawa
Swali la msingi.. Je Clouds TV mmeshapress charges against Makonda?MAKONDA AVAMIA CLOUDS KWA MITUTU YA BUNDUKI : [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] CHUPUCHUPU KUUAWA.
Jengo la Clouds Media Group lililopo Mikocheni B jana lilishuhudia sekeseke la aina yake baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuvamia akiwa na Walinzi wenye Bunduki.
Tukio hilo tukoea majira ya Usiku wakati kipindi SHILAWADU kikiwa hewani ambapo Makonda alivamia kwa lengo la kushinikiza Shilawadu waonyeshe mahojiano yenye lengo la kumchafua Askofu Gwajima.
Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba, mwanzoni wiki 2 zilizopita, SHILAWADU walipigiwa simu na watu wasiojulikana wakieleza kwamba wana 'ubuyu' mzito wa kuhusu Askofu Gwajima na mwanamke anayedaiwa kuzaa nae. Mwanzo Shilawadu walikataa habari hiyo, lakini siku moja walikutana na Makonda akawashawishi SHILAWADU wafuatilie stori hiyo. Kama kawaida yao kupenda umbea, SHILAWADU wakiongozwa na Soudy Brown walimtafuta mwanamke anayedaiwa kuzaa na Gwajima kisha wakamhoji.
Hata hivyo, kwa kuhofia nguvu ya Gwajima katika kupambana na shutuma dhidi yake, na kwa kuzingatia maadili ya kazi, SHILAWADU waligoma kurusha habari hiyo hewani mpaka wapate kauli za upande wa pili ( upande wa Gwajima ). Baada ya kuhangaika huku na kule , SHILAWADU walishindwa kupata upande wa pili wa habari ( walishindwa kubalance story ).
Kutokana na hilo, na kujua kwamba Gwajima asingewaacha salama kwa kutoa story ya uongo dhidi yake, [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] na wasimamizi wa vipindi wa Clouds Tv waliamua kuachana kabisa na story hiyo.
MAKONDA ANAINGIAJE? : Imefahamika kwamba watu ambao walipiga simu kwa Shilawadu kuhusu uwepo wa Mwanamke huyo ni watu wa Makonda. Makonda alitaka story hiyo itolewe kupitia [HASHTAG]#SHILAWADU[/HASHTAG] ambao wana kawaida ya kuripoti matukio ya Watoto/wanawake waliokataliwa. Kwa kuwa Makonda ana marafiki wengi pale Clouds, aliamini kwamba story hiyo lazima ingetolewa na hivyo kumchafua adui yake GWAJIMA ( kuzima sakata la vyeti ).
Akiwa nyumbani kwake Masaki, Makonda alikaa kwenye Tv yake Ijumaa kusubiri SHILAWADU wamvue nguo Gwajima. Cha kumsikitisha, Makonda alipata habari kwamba SHILAWADU wamegoma kupeleka habari hiyo. Hata viongozi akiwemo swahiba wake Ruge walikaataa kabisa kupeleka habari ambayo haiko 'balanced' na mbaya zaidi inawaingiza kwenye vita na mtu wa aina ya Gwajima.
Kama kawaida yake, Makonda aliamua kutumia ubabe. Kwa kuwa amezoea kuingia Clouds, Makonda alifahamu kuwa muda huo viongozi hawapo na watu waliopo anawamudu. Hivyo aliamua kwenda Clouds kuhakikisha Shilawadu wanaonyesha habari hiyo ya kumchafua Gwajima. Hivyo alibeba wanaume zaidi ya 8 wakiwa wamebeba silaha za moto.
Alipofika Clouds, walinzi wa Getini walimruhusu kupita yeye na gari iliyokuwa nyumba yake akisema ni rafiki zake wamekuja mara mara moja kwenye SOSOO FRESH kwani Adamu Mchomvu amewaalika. Lakini alipofika Reception, Mlinzi wa zamu alisitia baada ya kuona Makonda amekuja na watu wengi. NA HAPO NDIPO KASHESHE ILIANZA.
Walinzi wa Makonda walitoa Bunduki, walimtishia Mlinzi wakampiga sana na wakatumia nguvu kubwa hadi walifanikiwa kuingia ndani. Walipofika na Bunduki zao, Makonda aliamuru kila mtu kukaa alipo huku akilazimisha habari ya Gwajima iende. Kwisa kama kiongozi wa kipindi ndiye ambaye alipingwa mitama na ngumi za kutosha.
Kwa walioangalia kipindi wanajua kwamba kipindi hakikuisha, hiyo ni kutokana na kwamba Makonda na waligawa kipigo cha maana kwa Shilawadu kisha wakawabeba kwenda nao nje akisema wanaenda Cental.
Pia alitumia Bunduki kuwalazimisha Shilawadu wampe Video ya Mama anayedaiwa kuzaaa na Gwajima ( alipewa ). Makonda aliwaambia wapambe wake kama Shilawadu wamekataa kuonyesha habari hiyo baasi yeye atahakikisha inasambaa kupitia mitandao ya kijamii.
Hivi sasa Shilawadu hawako sawa kisaikolojia huku Suod Brown akiwa hana amani kwani alipigwa picha na Makonda alimuambia kama anaogopa kumdhalilisha Gwajima baasi yeye atadhalilishwa kwani Sura yake itawekwa hadharani kila mtu afahamu.
Baadae Makonda aliondoka baada ya kupigiwa simu ambayo haijulikani nani alipiga lakini Makonda alipoondoka Ruge alingia Clouds akiwa na watu huku na yeye amebeba bastola. Inaaminika ile simu ilipigwa kumuambia aondoke maana Ruge anakuja.
Source : Hidden.
Acha matusi na dharau soma vizur kipindi cha shilawadu kinarushwa ijumaa sasa yeye akwambie alhamisi ili iweje? Nyie ndo wakina bashiteWewe Ni demu???
Mbona usilete huu uzi tangu hiyo alhamisi??
Huyo ni Mrs daudi asikuumize kichwa tehe tehe teheAh! coco bhana... najua unajikaza ki-soap tu hapo, huna lolote!!! Ukibeba mzigo ukakuzidi nguvu; unaudondosha tu... simple! Back then, mwenzako nilikuwa namteteaga Bashite humu lakini hili zigo la safari hii nilipoliona tu; kwa mbaaaaaaaaaaaaali; nikajua ni zigo la misumari hili; halibebeki!!! Mwenzako mapeeeeeeeeeema; since day one nikasema hili la safari hii ni lako peke yako; na wala sitakaa kimya... nitakuwa nakutandika barabara as if sijawahi kukutetea huko nyuma!!!
Kwahiyo endelea tu kujikaza ki-soap! Chozi likikukaba liachietu hata kwa mayowe na nitakubembeleza!!!
Ndiyo maana ya Magu kumteua mtu wa kanda yake ili wamtumie wanavyotaka. Mkuu wa majeshi akinyamazia hili basi jibu tutakuwa tumelipataSwali la kujiuliza ?
Wale jamaa waliovaa ngwanda ni polisi?
Kama ni askari wa JWTZ basi jeshi limeoza...!
Nani anaevaa nguo za mabaka tanzania? Basi alikuja na Majambazi. Atuambie ni nani hao aliowavalisha uniform za kijeshi?? Na mamlaka hayo kayapata wapi??Una uhakika alikuwa na wanajeshi wa JWTZ?
Hivi hiyo clip imetolewa na Clouds au staff mmoja ameivujisha? ndo nawasha kimeo changu hapa msishangae swali languNatamani faru asimtumbue makonda amuache tu aendelee kumvua nguo, akitoka huyu mengi hatutayajua, na waswahili wanasema ukimchekea sana mbwa atakufata mpaka msikitini, ni yanayowapata clouds kwa sasa, huyo ni mbwa wao wenyewe,
Kingine walichogundua hawa clouds moto waliokuwa wameuwasha ulikuwa mkubwa walijua mange hatawaacha salama, na gwajima asienyamaza angewavua vibaya, wamepima faida ijayo, wamegundua bashite ni kama mgonjwa wa kansa kufa lazima, sasa wamemtosa rasmi, hii video haijavuja imetolewa rasmi na clouds kujisafisha