Rc Makonda na Steve Nyerere matatani, Msanii wakazi kumuandikia barua Rais kuwashitaki kwa kutowapa wasanii mwaliko maalum kwenda Leaders Club

Rc Makonda na Steve Nyerere matatani, Msanii wakazi kumuandikia barua Rais kuwashitaki kwa kutowapa wasanii mwaliko maalum kwenda Leaders Club

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wasalaam
Msanii Wkazi Muziki anapanga kumuandikia barua Rais Magufuli barua kuwashitaki Steve na RC makonda kwa kuwaita wasanii Leaders Club kupitia instagram..
Baada ya wasanii wachache kutokwenda Leaders wakilalamikia kuwa kamwe hawawezi kwenda sehemu kwa kujuzwa kupitia instagram hivyo waliihitaji mualiko maalum...

Steve nyerere aliulizwa na baadhi ya vyombo vya habari na kusema hata wao walipata kupitia insta na wakaitia wito na wakajuzana na hao wasiotaka kuja mpaka wapewe mualiko maalum wao ni kina nani? alisisitiza wao ni kina nani kuwashinda walio kuja mpaka wao pekee ndio wapewe mwaliko maalum? Aliendelea kusema alio waita allikuwa ni RC Makonda hivyo walipaswa kuitikia wito.

Baada ya kuambiwa wao ni kina nani mpaka wapewe mualiko maalum... Msanii wakazi aliandika mkeka kumjibu Steve..

Wakazi aliandika hivi

TOILET PAPER INAPO LICHEKA DODOKI!!

Moja ya vitu ambavyo vimeirudisha sanaa ya nchi yetu nyuma ni ufanywaji wa shughuli kiholela, kimihemuko, kwa maslahi binafsi, bila kujali PROFESSIONALISM. Inasikitisha STEVE NYERERE (Mpaka leo sijui ni msanii wa kitu gani, ila najua ni Mwana Siasa wa CCM kwa uhakika) kuwabeza watu ambao wamejaribu kusisitiza mambo kufanywa kiutaratibu unawaita Madodoki. Well, sir you are FULL OF SHIT, kama Toilet paper. Ilitakiwa uyavae mapungufu yako kama mratibu na kusema next time utafanya marekebisho sio kuwatukana. Mimi mwenyewe sikupata taarifa na ni moja ya wasanii ambao tupo very active kwa sasa. Mwaka Jana wakati Sekretariet ya Chama Cha Mapinduzi ilivyotaka kuongea na Wasanii, simu zilipigwa na mialiko ilitolewa na Humphrey Polepole. Sasa sisi ndio tushobokee kikao chako kisa Mkuu wa Mkoa, unaumwa nini?! Kwanza wewe na Mkuu wa Mkoa mna mandate gani ya kuongelea Sanaa wakati Waziri husika yupo (Mwakyembe) BASATA ipo, Shirikisho la Muziki lipo, na Vyama husika vipo. Msituletee mambo yenu ya holela holela hapa na agenda zenu binafsi kupitia Sanaa. Kwanza hamna jipya lolote mliloongea.

Kama mnataka kupeana michongo peaneni huko huko, muwaache wasanii tuendelee kutaabika na shida zetu. Uratibu wa Misiba sio sawa na Wa wasanii. Au nikuulize huyo Mkuu wa Mkoa anataka wasaidia wasanii wa Dar tu na Waliopo Instagram au?!
Mbona TCRA walitoa wito kwa wasanii kwenda kwenye kikao, wiki nzima na walitumia viongozi wa vyama?! Kuweni Professionals, na fanyeni mambo kiutaratibu kama kweli ni kwa maslahi ya wote, ila kama ni michongo yenu fanyeni kimya kimya kama ilivyo kawaida. Na mkiniudhi nitamuandikia Barua Rais Magufuli kuwasemea..!!
 
Safi sana!yaani mtu na akili zake kweli uitwe na Bashite uende?mtu ambaye ameichafua nchi kwa kola nyanja.Ccm kutpitia katibu mkuu walishasema hawatawatumia wasanii tofauti na TOT na Vijana band.Eric Shigongo kadhulumiwa na ccm mpaka leo Wema ana kesi za kubambikwa na huyo huyo Bashite

Lizaboni
 
- Vyombo vipo vya kusimamia sanaa na wasanii. Hili inabidi lizungumzwe na BASATA kuliweka sawa. Kunapoelekea wasanii wanaweza kuanza kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na kutengeneza makundi.

- Wasanii wapewe heshima zao na wathaminike kwani mchango wao ni mkubwa sana katika jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani mwaliko maalum ilikuwa lazima
 
- Vyombo vipo vya kusimamia sanaa na wasanii. Hili inabidi lizungumzwe na BASATA kuliweka sawa. Kunapoelekea wasanii wanaweza kuanza kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na kutengeneza makundi.

- Wasanii wapewe heshima zao na wathaminike kwani mchango wao ni mkubwa sana katika jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
kwani alikuwa ana kosa nini kwenda pale?
 
Back
Top Bottom