PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 459
- 644
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Charles Makongoro Nyerere, ametoa wito kwa wananchi Mkoani humo kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba 2025 kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema kila raia mwenye sifa ana haki na wajibu wa kushiriki katika uchaguzi huo, akisisitiza kuwa ni wakati wa kuamua kwa amani mustakabali wa Taifa letu.
Mkuu wa Mkoa amewahakikishia wananchi kuwa hali ya usalama katika Mkoa wa Rukwa ni shwari, na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika katika mazingira ya utulivu na ushirikiano.
Ametoa rai kwa wananchi kutanguliza amani, utulivu na mshikamano akisisitiza kauli yake, “Tuchague kwa amani, kwa sababu amani ni urithi wa kizazi kijacho.”