Uchaguzi 2020 RC Mbeya adai vijana 150 kuvuruga uchaguzi

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema serikali ya mkoa huo imejipanga kukabiliana na vijana 150 walioandaliwa kila Kata na vyama vya upinzani kwa ajili ya kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura siku ya Oktoba 28,2020, wakati wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 23, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, na kuelezea hali ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo amesema wanazo taarifa za makundi hayo kupanga njama za kufanya maandamano, kufunga barabara na kuwafanyia vurugu wasimamizi wa Uchaguzi kwenye vituo.

"Inasemekana kwamba kuna baadhi ya vijana 150 ambao wameandaliwa katika kila Kata, ambao watakuwa wanazunguka na bodaboda kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kutishia wapiga kura na kuufanya mji uonekana hauna amani, niwaombe wananchi amkeni Alfajiri mkapige kura na mkimaliza mrudi nyumbani", amesema RC Chalamila

Aidha amewahamasisha wananchi kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura na kwamba mara baada ya kukamilisha zoezi hilo warudi nyumbani kuendelea na majukumu mengine na kutokubali kubaki vituo kwa madai ya kulinda kura kwani sio jukumu lao.
 
Aseme tu, "Tumeandaa vijana 150 tumewapa kadi za CHADEMA, tumewapa kiasi cha fedha, maelekezo ni kuwa wajifanye wanafanya vurugu, kisha watakamatwa polisi, watawasachi na kutoa vitambulisho vya CHADEMA, watapelekewa mahabusu kisha tutawatoa kwa "dhamana"" na mchezo utaishia hapo
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, amesema serikali ya mkoa huo imejipanga kukabiliana na vijana 150 walioandaliwa kila Kata na vyama vya upinzani kwa ajili ya kufanya vurugu kwenye vituo vya kupigia kura siku ya Oktoba 28,2020, wakati wa uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.

Kauli hiyo ameitoa Oktoba 23, 2020, wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, na kuelezea hali ya ulinzi na usalama kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo amesema wanazo taarifa za makundi hayo kupanga njama za kufanya maandamano, kufunga barabara na kuwafanyia vurugu wasimamizi wa Uchaguzi kwenye vituo.

"Inasemekana kwamba kuna baadhi ya vijana 150 ambao wameandaliwa katika kila Kata, ambao watakuwa wanazunguka na bodaboda kwenye vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kutishia wapiga kura na kuufanya mji uonekana hauna amani, niwaombe wananchi amkeni Alfajiri mkapige kura na mkimaliza mrudi nyumbani", amesema RC Chalamila

Aidha amewahamasisha wananchi kujitokeza kwenye vituo vya kupigia kura na kwamba mara baada ya kukamilisha zoezi hilo warudi nyumbani kuendelea na majukumu mengine na kutokubali kubaki vituo kwa madai ya kulinda kura kwani sio jukumu lao.
Hivi kumbe Mbeya vituo vitafunguliwa alfajiri!!!???
 
Hao ni vijana aliowaandaa yeye ili wafanye fujo kisha wakamatwe chadema hii ni mbinu ya kiprimitive Sana.
 
NEWZ ALERT!!

Hao vijana wameandaliwa na CCM wenyewe. Wamehamasishana kwamba CCM wakapige kura asubuhi na mapema halafu ikifika saa 7 mchana hao vijana waanze kuleta chokochoko assuming kwamba CCM wote washapiga kura.

Chukueni tahadhari nchi nzima
 
Kwa njia hiyo siku ya uchaguzi hakuna kumpisha mtu awe mzee, mjamzito maana wengine wanaweza kuvaa matambala na kupaka unga waonekane wazee na wengine wajifanye wagonjwa yaani ukienda kupiga kura usimuonee mtu huruma unaingizwa choo Cha kike au Cha kiume.
 
Back
Top Bottom