RC Mrindoko: Ufyekaji wa Mahindi ya Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika si maelekezo ya Serikali

RC Mrindoko: Ufyekaji wa Mahindi ya Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika si maelekezo ya Serikali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

View: https://www.youtube.com/watch?v=gLonjJFJotY



Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,amesema kitendo cha wakulima wa wilaya ya Tanganyika kufyekewa mahindi kwenye msimu huu wa kilimo sio maelekezo ya serikali na si haki kufanya hivyo.

Mwishoni mwa mwezi Disemba,2024 baadhi ya wakulima wa kijiji cha Kagunga kata ya Kasekese wilayani humo walifyekewa mahindi yao zaidi ya hekari 60 na kutafsiriwa kuwa ni udhoroteshaji wa makusudi wa jitihada za serikali za kuifanya nchi kuwa ghala la chakula Afrika na kutokomeza janga la njaa.

Kiongozi huyo wa juu wa serikali ya mkoa, akizungumza hivi karibuni amebainisha pamoja na nia nzuri iliyopo ya kufanya doria katika misitu, maeneo tengefu na maeneo yaliyo hifadhiwa lakini ufyekaji wa mazao haukubaliki.

Ikumbukwe kuwa katika tukio la ufyekaji wa mahindi, Mkuu wa wilaya ya Tanganyika mkoa wa Katavi Onesmo Buswelu alisema mahindi yaliyofyekwa katika doria hizo ni mahindi na bangi ambazo zililimwa na wavamizi wa misitu.

Pia soma ~ Katavi: Wananchi Tanganyika walalamika kufyekewa mahindi hekari 60
 
Back
Top Bottom