Mlalamikaji daily
JF-Expert Member
- May 19, 2014
- 744
- 1,621
Najua unajua wazi kuwa Mkuu wa Mkoa yupo chini ya waziri, ama kwa lugha nyingine waziri yoyote yule ni boss wako wewe, kumtaja waziri wazi wazi kana kwamba si kitu, sio jambo jema.
Unaposema waziri akiuliza kuhusu makambi "wamjibu kwa kumuuliza kuwa watoto wake yeye wanasoma wapi?" unajua fika kuwa hii kauli ni wewe unayeuliza kwa huyo "waziri" indirect, maana hakuna RAIA mwenye uwezo wa kujibizana na waziri wazi wazi, wadau wa mambo wanasema hii ni kauli yako ya pili kutaja "waziri" katika namna ambayo binafsi sikuona kama inafaa.
Nakujua wewe ni mjenga hoja mzuri, na kuhusu kauli yako hii ya makambi niseme wazi kuwa una NIA NJEMA sana! kuinua elimu yetu nchini na hususani kwa mkoa wako! sasa twende sawa hapa! ILANI YA CCM INASEMA ELIMU BURE! na wazazi wanapigwa marufuku kuchangishwa michango inayoitwa ya hovyo hovyo! nadhani ikiwemo na hii ya makambi!
lakini pia, muda huo wa ziada kwa walimu hao unaangaliwaje? nani atakaye walipa walimu hao muda wa ziada posho? ama utawashurutisha walimu kwenye hayo makambi?
Lakini je NJIA PEKEE YA KUJIANDAA KWA MITIHANI NI KUWEKA KAMBI? kwamba bila kuweka kambi watoto hawawezi kufaulu? binafsi naona hapa mzigo huu unaangukia kwa wazazi na walimu! Mheshimiwa najua una nia njema lakini kumbuka ule msemo kuwa "SHAUKU ILIYOPITILIZA HAIUI PANYA PEKEE" asante.