RC Mtaka, una nia njema lakini...

RC Mtaka, una nia njema lakini...

Mwanafunzi asome miaka saba tunampima kwa mtihani wa masaa matatu akifeli mbumbumbu, mjinga hana akili.
Akitoboa hapo anasoma miaka minne anapimwa tena kwa mtihani.

Much as i respect mtaka as a leader makambi lengo lake ni yale masaa matatu tu mtoto afaulu, then what!!??
Tunahitaji mabadiliko kwenye mfumo wetu wa elimu, kuwe na continues assessment za wiki, mwezi hadi mwaka za kumpima mwanafunzi na matokeo yake kwa mwaka yaamue kufaulu au kufeli kwa mwanafunzi.
Tuwe na lugha moja ya kufundishia / medium of instruction from nursery to university.
NB: Ndalichako ni 🚮🚮 ndo anayefanya wasomi wadharaulike nchii hii, idara ya ukaguzi iboreshwe mwalimu afundishe idadi iliyokubalika, kama shule haina walimu na walimu mmewajaza mitaani hamuwaajiri kwanini tusiseme wewe ni 🚮🚮
Lastly tamisemi ndo wamiliki wa shule zote nchini nanyi ni 🚮🚮🚮mnaruhusu vipi shule ifunguliwe na hamna walimu maafisa elimu wilaya na mikoa nanyi ni 🚮🚮🚮🚮
 
Mtaka ni Mtu wa Mara..Kule Mara Kisu kinaitwa Kisu na hata Gari inaitwa Gari hivyo hivyo...Nchi imejaa wanafiki hii kama husimamii unachokiamini wewe hujui unaishi kwa ajili ya Nini...Kipindi cha Magufuli Wakuu wa Wilaya walikua wanakamata sana watu hovyo hovyo yeye Alikataa ujinga ule Mkoa aliokua anauongoza....Msimsakame kwasbabu ya Jamii yetu hii iliyojaa unafiki...

Tukirudi kiuhalisi ni Waziri Gani mtoto wake anasoma Hizi shule za Umma?? Wanasiasa wanajua darasa ndio elimu...Kwenye elimu kuna janga kubwa sana... Kubwa Sana Mm nimeona mtu kamaliza la Saba hajui hata Kuandika Jina...Huku Kuna janga ni kubwa mnoo...
Ni kabila gani?.
 
Hoja ya makambi na kukaa sana shuleni haina mashiko na inapingana na waraka wa elimu unaohusu muda wa masomo;

Watoto wanatakiwa kurudi nyumbani mapema kushiriki shughuli za nyumbani na kupata mapumziko na muda wa michezo. Hii ya kung'ang'ania watoto kukaa shule mpaka saa 11 ni ujinga, haina tija na inaandaa wazazi wasiojua shughuli za jamii mbeleni.

Mtaka kule Simiyu kilichomfanya aonekane bora sana ni ukosefu wa MEDIA (ulimuokoa sana), sasa hapo alipo ndio tabia yake halisi itajionesha vyema.
 
Back
Top Bottom